AMA kweli dunia sasa inaserereka! Katika hali ya kusikitisha, baba mzazi mwenye familia ya watoto watatu, mkazi wa Kambi ya Fisi jijini hapa, anashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kumbaka binti yake wa kumzaa hadi mtoto akafungua kinywa na kusema: “Nimechoka kubakwa na baba.”
Tukio hilo lililobumburuka hivi karibuni limewaacha watu vinywa wazi kwa sababu mtoto huyo ana umri wa miaka minane na kwamba alianza kufanyiwa ukatili huo mwaka jana akiwa na umri wa miaka saba alipokuwa darasa la pili katika shule moja ya msingi jijini hapa (jina tunalo).
AFUMWA LAIVU!
Inadaiwa kwamba mtuhumiwa huyo aliyetajwa kwa jina moja la Pelejai (34) ambaye ni mfanyabiashara wa mkaa, amemwingilia mwanaye huyo kwa mwaka mmoja.Taarifa zinasema, mwaka jana baba huyo aliwahi kufumwa laivu na mkewe akimtendea ubaya huo binti yake huyo.
Hata hivyo, inasemekana kuwa baada ya kunaswa chumbani kwake na mtoto, alimuomba msamaha mkewe ambaye alimsamehe kwa sharti la kutorudia tena kufanya tendo hilo la aibu na jambo hilo likawa siri kati yao.
Akizungumza kwa uchungu na gazeti hili akiwa katika Hospitali ya Mkoa ya Mount Meru anakopatiwa matibabu, mtoto huyo alisema chanzo cha baba yake kumbaka ni baada ya mzazi huyo kugombana na mama yake ambaye aliondoka nyumbani na kwenda kwao.
MARA YA KWANZA
Alisema mara ya kwanza kuingiliwa na baba yake alisikia maumivu makali mno huku akitokwa na damu nyingi.
Alieleza kuwa alijaribu kulia na kupiga kelele usiku huo lakini baba yake alimziba mdomo ili asitoe sauti.
Alisema alipomaliza kumfanyia ‘unyambilisi’ huo alimtishia kuwa endapo atasema popote, yeye atakamatwa na kufungwa na wao watabaki bila baba, hivyo watateseka kwa njaa.
Baada ya muda mtoto huyo alieleza kwamba baba yake huyo aliendelea kumwingilia mara kwa mara wakati kaka yake mkubwa wanayeishi naye akishindwa kusema baada ya kupewa fedha na baba yake.
MY GOD! KITANDA KIMOJA!
Alisimulia zaidi mtoto huyo alisema kwamba alikuwa akilala na baba yake kitanda kimoja kila siku kama mke na mume katika kipindi ambacho mama yake alipokwenda kijijini kwao Nduruma wilayani Arumeru kujifungua na kukaa kwa zaidi ya miezi mitatu.
“Ukweli nilichoka kubakwa na baba yangu lakini chanzo cha yote ni mama kutokuwepo nyumbani,” alisema mwanafunzi huyo.
Kwa upande wake, mama mzazi wa mtoto huyo alisema kuwa aligundua tukio la kubakwa kwa mwanaye tangu Machi mwaka huu na baada ya tukio hilo mumewe alimwomba tena msamaha kwa mara nyingine na yeye kumsamehe.
Mama huyo alisema kwamba alilazimika kwenda nyumbani kwao baada ya ujauzito aliokuwa nao kuwa mkubwa.
Alisema baada ya kujifungua aliendelea kuishi huko hadi Novemba 28, mwaka huu alipolazimika kurejea na kichanga chake baada ya kupata taarifa za kupotea kwa mtoto wake huyo anayedaiwa kubakwa na baba yake.
Alisema aliporejea nyumbani kwake Kambi ya Fisi alimuuliza mtoto wake mkubwa iwapo baba yake alirudia tabia ya kumbaka mwanaye lakini mtoto huyo hakusema chochote.
Akiwa anatafakari sehemu alipokuwa mwanaye ndipo alipopata taarifa kwamba alikuwa kituo cha polisi alikopelekwa na walimu wake baada ya watoto wenzake kutoa taarifa kwa walimu kuwa mwanafunzi mwenzao amekuwa akibakwa na baba yake mzazi.
SHULENI
Mmoja wa walimu katika shule hiyo alithibitisha kubakwa kwa mwanafunzi huyo baada ya kumhoji na kumkagua na kugundua kwamba ameharibika sehemu nyeti na kuwa kama za mtu mzima.
HOSPITALINI
Mama wa mtoto huyo akisaidiwa na walimu walitoa taarifa kituo cha polisi na kupatiwa hati ya matibabu (PF-3) na kumpeleka Hospitali ya Mount Meru.
Mwalimu wa shule hiyo alisema baada ya vipimo, daktari alithibitsha kwamba mtoto huyo alibakwa na kuharibiwa sehemu zake za siri.
Baada ya taarifa hizo kulifikia jeshi la polisi, vijana wa Inspekta Said Mwema walimtia mbaroni mtuhumiwa huyo na kumfungulia kesi ya ubakaji kwa hati ya mashtaka AR/RB/16064/2013-
UBAKAJI
Uchunguzi wa tukio hilo ukikamilika, mtuhumiwa atafikishwa mahakamani ili sheria ichukue mkondo wake.
INAUMA SANA!
Hivi karibuni kumeibuka vitendo vingi vya ubakaji na unyanyasaji kwa watoto, hivyo Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Sophia Simba na taasisi nyingine za utetezi wanaombwa kuingilia kati ili kuwanusuru watoto na ukatili huo
GPL
No comments:
Post a Comment