Najua ungependa kujua anacho kiwaza mtoto huyu akiwa kwenye usafiri wake mwenyewe alioubuni kiroho safi na kwa upeo wake mkubwa wa kufikiri. Labda ametengeneza kwa ajili ya kuendea shule au kumfikisha nyumba ya jirani kwa marafiki zake. Je kama wewe ndiyo kiongozi siwezi kusema wa nyazifa gani kwa bahati mbaya katika pita pita zako za kudai kula unamwona mtoto kama huyu unawezaje kumsahidia ili kipaji hiki kisiishie hapa hapa nyumbani?. Au na wewe utaomba ujaribu kuendesha na kujiringanisha kuwa ni mtoto. Tanzania inao watoto wengi kama huyu wenye vipaji kama hivi wanaoitaji kuendelezwa tu. Viongozi wetu tuache kumkimbiza kuku mweusi gizani, Mungu ibariki Tanzania, Ni mawazo yangu tu.
Hapa ni maeneo ya Kilole Korogwe Tanga,mtoto huyu alikutwa akicheza mwenyewe na baiskeli yake ya miti hana wasiwasi kabisa kiroho safi. Hapa ukute anawaza kutendeneza kitu cha kuruka kabisa au kitunza kumbukumbu.


1 comment:
Hii nidyo miaka 52 ya Uhuru tunayosheherekea. It is a big shame on all Tanzanian especially our leaders. God Bless that boy.
Post a Comment