Bi Winnie Madikizela Na Bi Graca Michel wote kwa pamoja wakifarijiana kwa machozi ya uchungu. Hapa ilikuwa siku ya mazishi ya Mzee Mandela huko Quru. Bi Winnie Madikizela ingawa ndoa yake na mzee Mandela ilisha fikia mwisho lakini unaweza kuona ni kihasi gani Mama huyu bado alikuwa na upendo ndani ya moyo wake. Na hapa analia kwa uchungu kwa vile anajua hawezi kumuona tena mzee Mandela aliyekuwa mume wake. Na mke wa mzee Mandela Mama Graca na yeye akilia kwa uchungu na wote kwa pamoja walifarijiana kama mtu na mdogo wake kama wanavyoitana wenyewe. Je mapenzi haya yataendelea au walishikamana kwa kipindi hiki kigumu tu?, Kila la kheli Bi Graca na Bi Winnie.
No comments:
Post a Comment