ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, December 31, 2013

NJEMBA YAGOMA KUSHUKA KUTOKA JUU YA MNARA WA SIMU UBUNGO JIJINI DAR AKIHITAJI KUONANA NA RAIS


Askari wa Kikosi cha Zima moto na Uokoaji Wakiwa wamepanda juu ya Mnara wa Simu Uliopo Ubungo Jijini Dar Es Salaam Muda mfupi uliopita kwaajili ya kumuokoa kijana mmoja aliyefahamika kwa jina moja la Hassan Ambaye alipanda juu ya mnara huo kwa lengo la kufikisha Ujumbe wa kutaka kuonana na Raisi Kikwete ili aweze kumwelezea kwa kile anachodai kuwa jeshi la polisi lilimbambikia kesi na hatimaye kuhukumiwa kifungo cha Miaka 6 kwenda jela


Askari wa Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji wakiendelea na zoezi la kumuokoa Kijana Hassan kwaajili ya kutojirusha kutoka Juu ya Mnara wa Simu Muda mfupi uliopita Ubungo Jijini Dar Es Salaam Leo


Hapa akishushwa na askari wa Kikosi Cha Zimamoto na Uokoaji

Hapa Askari wa Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji akiwa amemuweka begani na Kushuka nae chini Mara baada ya kufanikiwa Kumshika vizuri kwaajili ya kumteremsha chini bila kupata madhara

Kijana aliyefahamika kwa jina moja la Hassan akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kushushwa juu ya Mnara wa Simu na Askari wa Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji muda mfupi uliopita Ubungo jijini Dar

Tukio likiendelea huku wakazi wa jiji la Dar Wakiendelea kushuhudia.Picha Zote na Josephat Lukaza Wa Lukaza Blog



Raia wakishuhudia tukio hilo


Wakazi wa Jiji la Dar wakishuhudia tukio hilo lililotokea muda mfupi uliopita Ubungo Jijini Dar leo

Gari la Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji likiwa limetia timu eneo la tukio kwaajili ya Kuokoa

Wakazi wa Jiji la Dar wakishuhudia gari la Polisi likiondoka na Kijana Hassan ambaye alipanda juu ya Mnara leo Ubungo jijini Dar Es Salaam ASANTEL UKANZA BLOG

No comments: