ANGALIA LIVE NEWS

Monday, December 9, 2013

RAIS KIKWETE AWASILI PRETORIA KUHUDHURIA IBADA KUU (MEMORIAL SERVICE) YA KITAIFA YA MSIBA WA NELSON MANDELA

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa katika uwanja wa ndege wa Waterkloof Airforce Base ulioko Kusini mwa jiji la Pretoria alikowasili usiku wa kuamkia leo tayari kuhudhuria mazishi ya Rais Mstaafu wa Afrika Kusini Mzee Nelson R. Mandela.
Rais Kikwete akisalimiana na Mwambata wa Kijeshi katika Ubalozi wa Tanzania Afrika kusini katika uwanja wa ndege wa Waterkloof Airforce Base ulioko Kusini mwa jiji la Pretoria
Rais Kikwete akisindikizwa kuelekea kwenye gari baada ya kuwasili uwanja wa ndege wa Waterkloof Airforce Base ulioko Kusini mwa jiji la Pretoria . Nyuma yake mwenye ushungi kichwani ni Mama Salma Kikwete
Rais Kikwete akisindikizwa kuelekea kwenye gari baada ya kuwasili uwanja wa ndege wa Waterkloof Airforce Base ulioko Kusini mwa jiji la Pretoria . Nyuma yake kushoto ni Katibu Mkuu wa CCM Ndg Abdurahman Kinana. 

Rais Jakaya Mrisho Kikwete amewasili nchini Afrika Kusini usiku wa kuamkia leo  Desemba 10, 2013 tayari kuhudhuria maziko ya Rais Mstaafu wa Afrika Kusini Mzee Nelson R. Mandela.
Kwa mujibu wa taarifa rasmi ya serikali, Ibada Kuu ya kumwombea Marehemu itafanyika leo Desemba 10, 2013 katika Uwanja wa FNB Johannesburg, ambapo viongozi na watu mashuhuri mbalimbali kutoka kila pembe ya dunia wataungana na wananchi wa Afrika Kusini katika shughuli hiyo ya kihistoria. 
Kesho Novemba 11 hadi Novemba 13, 2013 mwili wa marehemu utakuwepo katika jengo la Union Building ambapo viongozi na watu mashuhuri watatoa heshima zao za mwisho. Jengo hilo ni kama Ikulu ya nchi hiyo.
Maziko yatafanyika Desemba 15, 2013 katika kijiji cha Qunu, Mthatha, Easter Cape

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete  atahudhuria Ibada Kuu ya Kitaifa (Memorial Service) ya msiba wa Rais Mstaafu wa Afrika Kusini Mzee  Nelson R. Mandela kwenye Uwanja wa Michezo wa FNB mjini Johannesburg.
Rais Kikwete anajiunga na mamia ya viongozi wa nchi mbali mbali duniani kuomboleza kifo cha mmoja wa viongozi mashuhuri zaidi duniani katika karne za 20 na 21.
Rais Kikwete ameambatana na Makamu Mwenyekiti wa Pili wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd na mkewe Mama Asha; Mama Salma Kikwete na Ndugu Abdulahramani Kinana, Katibu wa Mkuu wa CCM.
PICHA NA IKULU

1 comment:

Anonymous said...

msibani au kwenye sherehe, it is all smiles there!!