Baada ya kupokea barua
yake ya mashtaka 11 tarehe
01/12/2013 ambayo
anashitakiwa nayo na iliyomtaka ajitetee
kwa maandishi, Mheshimiwa Zitto Zuberi
Kabwe (MB) jana
tarehe 10/12/2013 amefanya hivyo kwa mujibu wa Katiba na
Kanuni za Uendeshaji za Chama.
Pia Mheshimiwa
Zitto Zuberi Kabwe (MB) ametoa taarifa kwa
Katibu Mkuu wa Chama kumueleza nia yake kukata
rufaa
Baraza Kuu la Chama kupinga hatua iliyochukuliwa na Kamati
Kuu dhidi yake kumvua nyadhifa zake ndani ya Chama.
Kuna sababu mbili za msingi za kukata rufaa;
1. Utaratibu wa kuchukua hatua za nidhamu ulikiukwa.
2. Sababu za kuchukuliwa hatua hizo sio sahihi.
Utaratibu ambao unatakiwa kufuatwa kabla ya kumchukulia
hatua za kinidhamu
kiongozi kwa mujibu wa Katiba na Kanuni
za Uendeshaji
ni kama ifuatavyo;
Kanuni ya Uendeshaji 6.5.6 inasema;
1
kwanza kupewa mashitaka
yake kwa maandishi na mamlaka
husika na kupewa nafasi ya kujibu mashitaka kwa maandishi.
Pia tunapenda
ijulikane kwamba Kanuni ya Uendeshaji 6.5.2
(a), (b), (c) na (d) kama ilivyorekebiswa Januari 2013 inasema;
Kwa mujibu wa ibara ya 5.4.3 na 5.4.4 ya Katiba mwanachama
yeyote hatachukuliwa hatua za kinidhamu ama kuonywa ama
kuachishwa ama kufukuzwa uanachama
bila kwanza;
a) Kujulishwa makosa
yake kwa maandishi na kutakiwa
kutoa
majibu katika muda usiopungua
wiki mbili.
b) Kupewa nafasi ya kujitetea
mbele ya kikao kinachohusika.
c) Mwanachama atajulishwa kwa maandishi uamuzi wa kikao
mnamo wiki mbili baada ya kusikilizwa.
d) Kamati Kuu inaweza kuchukua hatua za dharura bila
kuzingatia utaratibu (b), (c) hapo juu kama itaona maslahi
ya Chama kwa ujumla yanaweza
kuathiriwa isipokuwa
mwanachama au kiongozi anayelalamikiwa atalazimika
kuitwa kwenye kikao husika.
2
ulifanya mkutano na waandishi mnamo tarehe
26/11/2013 na
kusema kwamba marekebisho haya ya Kanuni ya mwaka 2013
ambayo nimewawekea hapo juu, ndiyo utaratibu waliofuata. Pia
walieleza kuwa sikuwa naifahamu na nilidanganywa kwani Kanuni
ilishabadilishwa. Mabadiliko haya ambayo ni katika kipengele
(d)
kuhusu hatua ya dharura
iliyochukuliwa na Kamati Kuu haikugusa
kipengele (a) cha Kanuni. Yaani ni kuwa hata kama Kamati kuu
itachukua hatua ya dharura
kwa mujibu wa kipengele (d), bado
kipengele (a) ni lazima
ifuatwe na inatamka wazi sharti la kiongozi
kupewa mashtaka kwa maandishi na kupewa
nafasi ya kujibu kwa
maandishi. Hii ni haki ya msingi kwa kila
utawala au uongozi.
Mheshimiwa Zitto Zuberi Kabwe hakupewa mashtaka yake aliyakuta
ndani ya kikao baada ya kupewa taarifa kwa ujumbe wa simu (text
message au sms).
Kwa uzito wa makosa hayo yaliyosababisha kuvuliwa uongozi na
kwa kuangalia athari
zake kwake yeye binafsi na chama
kwa
ujumla, Kamati Kuu ilitakiwa kujiridhisha kwamba Kanuni za
Uendeshaji na Katiba zinafuatwa.
Hili linaendana na utaratibu uliotumika kwa Samson Mwigamba
kuvuliwa nyadhifa yake ya uenyekiti wa mkoa.
Yeye hakuitwa
kabisa kwenye kikao hicho na ni ukiukwaji wa Kanuni ya Uendeshaji
Taarifa
kwa Vyombo vya habari 11/12/2013 Albert Msando 3
6.5.6(d) niliyoisoma hapo juu kwamba lazima kiongozi huyo aitwe
kwenye kikao.
Sababu zilizotumika
ingawaje hajapokea taarifa rasmi ya maandishi
kwa mujibu wa Kanuni za Uendeshaji ni kwamba yeye ameshirki
kwenye kuandaa
na kusambaza waraka ambao unasemekana ni
mkakati wa ushindi wenye lengo la kupindua uongozi
uliopo.
Waraka huo haukumtaja Mheshimiwa Zitto Zuberi Kabwe
kama
muandaaji au msambazaji. Waliouandaa hawajaukana na badala
yake wamesema waziwazi kabisa
kwa maneno na maandishi
kwamba Mheshimiwa Zitto Zuberi Kabwe HAHUSIKI. Sio sawa
kumuadhibu Mheshimiwa Zitto Zuberi
Kabwe kwa hisia au tu kwa
sababu ya urafiki wake na watu fulani.
Haya ni mapungufu ambayo kwa bahati nzuri Katiba na Kanuni za
Uendeshaji zinatoa nafasi ya kurekebishwa kwa kutoa nafasi
ya
kukata rufaa. Na utaratibu ni huu hapa;
Kwa ufupi, Ibara 6.3.6(d) ya Katiba ya Chama;
“Kiongozi aliyechukuliwa hatua za kinidhamu na mamlaka
yake ya nidhamu anayo haki ya kukata rufaa ngazi ya juu ya
ile mamlaka yake ya nidhamu na uamuzi
wa ngazi hiyo
utakuwa wa mwisho”.
4
“Rufaa yoyote lazima ifanyike
katika muda wa siku thelathini
tangu tarehe ya kupokea
rasmi kwa maandishi maamuzi ya
mamlaka iliyotoa adhabu”.
Kanuni za Uendeshaji zinatoa UTARATIBU ambao unatakiwa
ufuatwe ili kiongozi aliyeadhibiwa aweze kutumia HAKI yake ya
kukata rufani kwa maneno haya;
Kanuni ya 6.5.8 ya Kanuni za Uendeshaji;
“Kiongozi aliyeadhibiwa atapewa taarifa ya msingi wa
maamuzi ya mamlaka ya nidhamu ili kumuwezesha kuamua
kukata rufani au la”
Kanuni ya 6.5.9 ya Kanuni za Uendeshaji;
“Mwadhibiwa atakayeamua kukata rufani atatakiwa kufanya
hivyo katika muda
wa siku thelathini baada ya kuarifiwa
uamuzi wa adhabu”
Kanuni ya 6.5.10 ya Kanuni za Uendeshaji;
“Baada ya kutoa uamuzi kikao husika kinalazimika kuandaa
taarifa kamili ya mwenendo wa shauri
na kuwasilisha ngazi ya
juu. Taarifa hiyo lazima ifike katika
muda wa siku kumi na nne
baada ya kikao cha mamuzi”
5
Mpaka hivi sasa hatujpokea taarifa kamili ya mwenendo wa
shauri tokea kikao cha Kamati Kuu cha tarehe 20-21/11/2013
Huo ndio utaratibu ambao Mheshimiwa Zitto Zuberi Kabwe
ameamua kufuata
kwa kuheshimu maamuzi
ya Kamati Kuu
lakini kukatia rufaa maamuzi hayo. Kuheshimu maamuzi sio
kuyakubali uhalali wake.
Kumekuwa na matukio ya kusikitisha ambayo
mengine
yamefikia mahali kuwa fujo na vurugu
ikiwa ni pamoja na
kurushiwa mawe Katibu Mkuu wa Chama. Vurugu hizo baadhi
zimehusishwa na Mheshimiwa Zitto Zuberi Kabwe na baadhi ya
watu.
Mheshimiwa Zitto Zuberi Kabwe hahusiki kwa njia yoyote na
hayo yanayoendelea na anayakemea na kuwashauri
wanachama wote kuwa watulivu na kuendelea kuwaheshimu
viongozi wa kitaifa. Hatua zimeshachukuliwa kukata rufaa na ni
imani yake kwamba
Baraza Kuu la Chama litatenda haki kwa
kupitia rufaa yake na kutoa uamuzi.
Nawashukuru
wote.
ALBERT MSANDO, Mwanasheria
11/12/2013
No comments:
Post a Comment