ANGALIA LIVE NEWS

Monday, December 16, 2013

UNYAGO CHANZO CHA MIMBA ZA UTOTONI

Na Hamisi Magendela

WATANZANIA na Afrika kwa ujumla huwa wana tamaduni zao ambazo kwa namna moja au 
nyingine hadi zipo zinazodumishwa na kuendelezwa japo wakati mwingine zinakuwa zikiathili 
jamiio furani.

Lengo za tamaduni hizo ni kuelimisha, kuonya na wakati mwingine kuburudisha kwa nyakati 
maalum kwa kufanyika sherehe kubwa zinazoambatana pamoja na unywaji wa pombe na zaidi za 
kienyeji na ikisindikizwa na burudani ambayo wakati mwingine uchezwa hadi usiku na kukesha.
katika suala zima la ukeshaji katika shughuli za kitamaduni ni sehjemu moja ambayo inakuwa
inasababisha madhala makubwa katika jamii hasa watoto wa kike ambao wakati mwingine hapo 
ndipo wanapoitumia nafasi ya kufaya mambao ambayo yanakuja kuwaathiri siku za baadae.
hapo na nizungumzie tamaduni moja ambayo naamini kwa njia moja au nyingine ni sehemu ya 
inayosababisha matatizo kwa watoto wake muda mfupi baada ya taratibu za tamaduni kufanyika 
jambo ambalo inahitajika kazi ya ziada kuhakikisha elimu inatolewa ili kupunguza atahri 
zianazojitokeza baada ya hapo.
Unyago ni sehemu ya mila na destuli ya makabila mengi nchini Tanzania ambayo badao inatekelezwa 
na kudumishwa na lengo kubwa ni kuwapa elimu vijana wa kike kufahamu mambo mbalimbali 
kuhusu maisha ya ndoa na usafi juu ya mwili wake.
Aidha elimu ya Unyago inamfanya mtoto wa kike kujiandaa na maisha ya kuwa mama na kuweza 
kutunza familia atakayoweza kuwa nayo wakati ukifika wa kupata mwenza ambaye wataweza kuishi 
pamoja kama mke na mume.

Elimu hiyo utolewa kipindi cha likizo baada ya shule kufungwa hasa Desemba kutokana na kuwepo 
muda mwingi wa mapumziko ,ndiyo nafasi inayotumiwa na wazazi ama walezi kuwaweka ndani 
vijana wao wa kike kwa muda fulani na baada ya hapo utolewa kwa sherehe kubwa.
Lengo si kushawishi tamaduni hiyo kuondolewa bali ni koberesha kwa kuzingatia umri kuwaweka 
ndani na kuwapa elimu hiyo kwa maana wengi wao ni miaka 12 kitu ambacho ni mapema saa 
kuwapa elimu hiyo.

Wengi wa umri huo wanakuwa na tabia ya kufanya majabiribio ya tendo na kujikuta wakipata
ujauzito mapema kabla ya wakati na kuwasababibi9shioa kupata matatizo makubwa yakiwemo 
kushindwa kumwagika damu nyingi na kufariki, mama pamoja na mtoto au mmoja kati yao.
Pia usababisha kukosa masomo kwa kufukuzwa shule kutokana na kupata ujauzito kwa wakati huo 
na taswra ya maisha uanza kuharibika hapo kwa maana hata wazazi wanachukua nafasi kufukuza 
nyumbani msichana huo.

Fatma Shabani (27) ni miongoni mwa wanawake aliyepoteza usichana wake kipindi cha sherehe za 
unyago zikifanyika na kujikuta akipata ujauzito bila ya kujua.
Anasema kuwa wakati sherehe ya Mdogo wake, alikutana na mwanaume na kumlaghai kufanya naye 
ngono ilisababisha kupata ujauzito akiwa na miaka 15 ingawa hakuwa kusudio lake kupata ujauzito 
kwa wakati huo.

Japo alikiri mwaka mmoja nyuma alipata mafunzo ya unyago lakini anadai hayakumsadia lolote 
kutokana na kutozingatia maelekezo aliyokuwa akipewa kwa wakati huo.
Inawezekana umri wa wasichana wanaopata elimu hiyo ikawa ni tatizo, ndiyo maana vitendo vya 
ngono huwa vinashamili baada ya vijana hao kutoka katika unyago.

Pia inawezekana mila hii wakati mwingine ikawa ni chanzo kikubwa cha mimba za mapema kwa 
watoto wa kike hivyo ni vyema ikaangaliwa upya jinsi ya njia ya kutumia kuwafikishia elimu hiyo.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Mtwara Mikindani, Sabin Sirima, anaeleza kuwa tatizo la watoto 
kupata mimba linatokana na utamaduni wa eneo husika.

Nakubaliana na maneno hayo kwa mapana zaidi, kwani ukiangalia kwa makini, mikoa ya kusini 
imeathirika zaidi na tatizo la wasichana kupata ujauzito ukingalinisha na mikoa mingine ya hapa nchi 
kutokana na kuendeleza mila na desturi bila ya kuzingatia nyakati.

Ni vyema ili kuweza kuendana hali halisi ya maisha ilivyo sasa watoto wengi wanakuwa na uelewa 
na udadisi wa kujua mambo kwa haraka zaidi na kuyafanyia kazi licha kuelezwa kuwa wakati wa 
kufanya hivyo kwa rika lao bado.

Suala hilo limekuwa likiwafanya mabinti kuingia katika vitendo vya ngono mapema na kujikuta 
wakiwa katika hali mbaya baada ya kupata ujauzito ambao hawakuutarajia na kuwa mwanzo wa 
maisha yao kuharibika.

Hali hiyo hutokea pindi tu mtu aliyempa ujauzito kuingia mitini na ndoto ya kuwa maisha ambayo 
aliyafikiria kuwa kuwa na mwanaume kwa kipindi hiko ni sahihi kumbe ni hasara zaiodi kwa kipindi 
na majuto uanzia hapo. 

hiko ni kielelezo tosha kwamba baadhi ya mila hasa ya unyago kwa kiasi fulani inasababisha watoto 
wa kike kuwa ombaomba baada ya kacha shule kutokana na ujauzito na ikiwa atatelekezwa na
aliyempa ujauzito ndipo taswira ya maisha yake inapoanza kuharibika.

Kwa maana wengi wao wanakuwa bado wanafunzi wa shule za msingi na kusababisha kuacha shule 
kwa kupata ujauzito licha ya rais kikwete kutoa tamko la kuruhusiwa kuendelea na shule kwa 
wasichana wanaopata mimba wakiwa shule kutofanyiwa kazi ipasavyo.

Ally Makwilo mkazi wa manzese, anasema anaamini kuwa katika mikoa hasa ya pwani wamekuwa 
na kipaumbele cha utamaduni na si elimu jambo ambalo linalowaletea shida kuendelea kimasha 
kutokana na kutumia muda mwingi katika kuangalia lini watacheza ngoma ya mtoto ya kuwatoa 
wali, baada ya kupata mafunzo ya unyago.

Taarifa kutoka Tanga zilionyesha kuwa katika mkoa huo tatizo la wasichana kukatisha masomo ni 
kubwa zaidi. Mathalani, karibu wasichana 300 walikatisha masomo yao mwaka 2009 kutokana na 
mimba za utotoni kwa mwaka 2010) wakati Mkoani Kagera hali ni ileile, taarifa zinaonyesha kuwa 
wasichana 880 walikatisha masomo yao kutokana na kupata mimba wakiwa shule. (Jambo Leo: 
Januari 12, 2010).

Katika mkoa wa Pwani pekee karibu wasichana 500 walikatisha masomo yao kati ya mwaka 
2005-2009 kutokana na kupata mimba za utotoni (Jambo Leo, Machi 2010). Taarifa za Utafiti 
kuhusu mimba za mapema kwa wasichana uliofanywa hivi karibu na Chama cha Waandishi wa 
Habari Wanawake (TAMWA), zinatoa picha ya kutisha.
Mathalani, mkoani Tabora pekee wasichana wa shule 819 walipata mimba kipindi cha mwaka 
2006-2009. Na huko Morogoro kati ya mwaka 2007-2009 wasichana wa shule 331 walipata mimba 
na kukatisha masomo yao.
Takwimu za kitabu cha Takwimu za Elimu Tanzania (2005-2009) zinaonyesha kuwa watoto wa 
kike walioacha shule kutokana na mimba za utotoni ni wengi kiasi cha kuogopesha ambapo idadi ya 
wasichana waliocha shule kwa ujauzito zilikuwa 16,991kwa wakati huo.
Ukubwa wa tatizo kiujumla ni kubwa kuliko inavyoelezwa na inatisha, inaogopesha na inaamsha 
hisia za kuwajibika ki-ubunifu ili kuokoa kizazi cha watoto wetu wa kike, Wanawake ni sehemu 
kubwa ya jamii yetu ambayo mchango wao ni mkubwa katika taifa letu.
Halima Makangila, anasema katika Unyago vijana wa kike wanafundishwa masuala ya ndoa na 
kuwajenga kiakili, hivyo akili yao inajengeka kuwa wako tayari kuishi na mwanaume na kubeba 
ujauzito na kupata watoto.
"Si vyema masuala hayo ya unyago kuyaingilia moja kwa moja kwa maana yanagusa imani na
taratibu za watu katika kuendesha maisha tao ya kila siku, hivyo ni vyema elimu ikatolewa taratibu 
ili kuwashawishi walezi kuwaacha watoto wa kike wanapevuka wakiwa shule ya msingi kuwaacha 
hadi wanapomaliza elimu hiyo ili kuwaondolea adha wanayoweza kuipata baada ya kurudi katika 
unyago," alisema Makangila.
taratibu.

Ni ukweli kwamba serikali imekuwa ikijipanga kuahakikisha mtoto wa kike anafanya vizuri katika 
masdomo yake, lakini tatizo la mimba mashuleni ni kikwazo kikubwa kwa vijana hao wa kike 
kufikia kmalengo ya Serikali kwa maana wengi uolewa au kupta mimba na kutelekezwa.
Taasisi mbambali zimeliona tatizo hilo na kusababisha kutioa elimu ili kukabiliana na tatizo hilo ili 
kupunguza hali tete ya vijana wa kikae kupata mimba na kuwafanya kuwa tegemezi miongini mwa 
jamii inayowazunguka.
Hali hiyo imesaidia kwa kiasi kikubwa kubadili mwelekeo wa wanafunzi kuwa wakipata sekondari 
wanapomaliza msingi, wanakwenda. Kutokana na hali hiyo, hivi sasa wasichana wengi wanamaliza 
darasa la saba tofauti na ilivyokuwa awali.
Fatuma Kambi, aliyewahi kuwa Afisa Elimu Rufiji, alisema hali ilikuwa mbaya wakati anaanza kazi 
katika mkoa huo kutokana na wasichana wengi waliokuwa wakiacha shule kutokana mila ya Unyago 
ambayo ilishamili kwa kiasi kikubwa japo kwa sasa imepungua kiasi fulani.
"Siyo kwamba tunakataa mila hiyo isiendelee kwani kwa kufanya hivyo tunapkuwa tunaingilia uhuru 
wa mtu, kitu ambacho si kizuri hivyo tulikuwa tukiwashauri wawaache mpaka wamalize elimu ya 
Msingi japo baadhi ya wazazi walikuwa wakipuuza ushauri huo", alisema Kambi.
Kambi ambaye kwa sasa ni Mkurugenzi wa Ufundi katika chama cha Walimu Wanawake Tanzania, 
alisema kwa sasa kupitia Vikundi mbalimbali kwa pamoja wamekuwa wakitoa elimu kwa wazazi ili 
waweze kuwa waelevu katika Muda wa kuwafanyia mabinti hao Mafunzo ya Unyago.
Anasema hali ni mbaya kwa wasichana ikiwa elimu kuhusu Unyago haitatolewa vizuri kwa 
kuzingatia muda wa watoto hao kwa maana ikiwa watafanyiwa mapema kuna hatari ya watoto wa 
kike wakawa masikini na tegemezi kwa kukosa elimu ya kuwatoa katika hali moja kwenda nyingine 
ya kimaendeleo.
"inaumiza kuona wasichana wetu wakiaharibu maisha yao wakiwa katika umri mdogo, baada ya 
kupata mimba wakiwa watoto na hawafahamu nini cha kufanya baada ya kukimbiwa na mtu 
aliyempa ujauzito na kuwa chanzo cha hali ya maisha kuharibika", alisema Kambi.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa kikundi cha Mwangaza Sanaa cha Manzese Dar es Salaam 
Addsony Mgeni, anasema tatizo la mimba kwa wasichana wenye umri mdogo linatokana na mila na 
desturi inachangiakutokana na kuyafanyia majaribio yale waliofundishwa kweny unyago.
Pia anasema kuwa inatakiwa kutoa elimu taratibu ili watu waweze kuondokana na desturi ya 
kuwacheza ngoma wasichana wakiwa na umri mdogo kwa njia moja au nyingine itasaidia 
kupunguza tatizo hilo kama si kumaliza kabisa.
Nkya anasema wengine waliopata ujauzito walidanganyika kwa kupewa msaada wa usafiri kutokana 
na shule kuwa mbali na makazi ya watu hivyo na kubaini wanafunzi wengi wanatembea umbali 
mrefu hadi kilometa 20 kwenda shule.
“Tatizo la shule kuwa mbali lingeweza kuepusha mimba iwapo shule zingekuwa na mabweni kwa 
ajili ya wanafunzi wanaoishi mbali na shule,”alisema.
Alisema mfumo wa elimu ubadilike gharama ya elimu itoke katika mfuko wa serikali zisitumike 
fedha za wazazi hivyo kila mtoto wa kike na kiume wanatakiwa wapate elimu bure.
Kwa mujibu wa taarifa za Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi katika kipindi cha mwaka 2004 
hadi 2008, jumla ya wanafunzi 28,590 wakiwepo 11,599 shule za msingi walikatishwa masomo 
kwa kupata mimba.
Nkya anasema taarifa mikoa iliyofanyiwa utafiti ni Dar es Salaam, Morogoro, Iringa, Mbeya,
Dodoma, Kigoma, Mwanza, Mara, Shinyanga, Tanga, Kilimanjaro, Tabora, Lindi, Ruvuma, Manyara 
Kaskazini Pemba na Kusini.

2 comments:

Anonymous said...

Napenda kutoa machecho kutoa na huyu mwenzetu alivyozunguamza kuhusu UNYAGO. Kwanza ningependa uelewe unyago hawafundishi kufanya mapenzi tu,wanamfundisha mwanamke kuwa mwanamke bora na pia kuweza kulinda familia yake. kuhusu kupata mimba hiyo sio kweli tatizo la mimba lipo kila kona dunia hii na sababu kubwa ni kukusa maadili ambayo wewe ndio unayapinga. Hata wanaume nao wanatakiwa kufundwa maana wanaume wengi wa sikuizi hawajui hata nini maana ya kuitwa mwanaume wanazania ni kuota ndevu na kukimbia majukumu.

Anonymous said...

acheni zenu watu wanafuata mila zao leo hii mnawaletea maneno yenu ya kinafiki na umbeya wa magazetini kwanza mwenye akili timamu angaliye kichwa cha habari na kutafakari, mtoto ni waiana gani na tafsiri ya mtoto katika kamusi uangaliye na pia kushika mimba ni jambo gani.

ukishakushika mimba basi si mtoto tena msitulete zenu za kinafiki za kibara bara vijijini watu wadaa tunakula raha na mila na desturi zetu za unyago wazaramu wote oyeeeeeeeeeeeeeeeee