ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, January 4, 2014

ARTIST MTANZANIA AISHIYE CHICAGO KU-RELEASE TV VERSION YA VIDEO YAKE “ALL I HAVE”


Baada ya msanii Ardo King ku-release single yake aliyoibatiza jina la  “ALL I HAVE” aliyomshirikisha Passion ambayo imeweza kukubalika vizuri kwa kuonyesha ukomavu wa style na lyrics katika kila sikio la wapenzi wa muziki huu waliowahi kuisikiliza. Hivi sasa ameamua kurelease Tv Version ya video yake mpya ambayo inaanza kurushwa katika vituo vya Television mbali mbali katika nchi kadhaa za bara la Afrika ikiwemo Tanzania mwanzoni mwa mwaka huu 2014. 

Akiongelea sababu zilizo pelekea kutoa TV version licha ya kuwa alishatoa video ya wimbo huo ambayo pia inapatikana YOU TUBE, alidai kuwa ni kutokana na kutoridhika na kazi ile ya awali na alikuwa na malengo zaidi ya hapo na hivyo hakuona umuhimu wa kuishia hapo. “Kutokana na kubanwa na shughuli za kimaisha unaweza kujikuta hupati muda muafaka wa kusimamia shughuli za editing na mixing za kazi yako, so mara nyingi wavivu hupenda kutumia gap hilo kulipua kazi na kujipatia cash ya fasta, by the way nili-fly to bongo mara baada  ya ku-shoot video, so hiyo iliplay a huge part too” aliongeza.

Katika jitihada za kuiboresha kazi, aliamua kusubiri hadi hapo alipokuwa na muda muafaka na kukamata usukani mwenyewe na kuanza kuisuka kazi upya from the scratch kitaalamu, kuchanganya vionjo mbali mbali na kutumia vifaa/technology za kisasa na bora zaidi. Ardo King ambaye pia ameshawahi kumiliki Audio na Video production studios nchini Tanzania amekuwa na uzoefu wa muda mrefu hivyo hakuona haja ya kumuajiri mtu kufanya kazi hiyo ambayo anaweza kuifanya tena kwa ufanisi zaidi akipata muda wa kutosha.
Ardo King pia alidokeza kiasi kuhusu project yake ya pili ya video ya single yake ambayo ni ya lugha ya Kiswahili aliyoifanya na Kampuni anayoshirikiana nayo kwa hivi sasa, Legendary Music Tanzania na hapa US. Habari zaidi zitapatikana hapa mara mambo yatakapokuwa tayari. Alipoulizwa dream yake kubwa ni nini katika Sanaa hii ya muziki alikudai ni ku-grow big na kuongeza fans daily.

No comments: