Kwa mujibu wa wakazi wa eneo hili la Jang'ombe, mjini Zanzibar wanaeleza kuwa eneo hili ambalo kwa sasa limebaki wazi na kuwa historia huku likiogopwa na kila mmoja, lilikuwa ni bonge ya shimo kubwa lenye urefi zaidi hata ya mita mia baada ya nyumba iliyokuwa eneo hili kuzama nzima nzima na kila kitu kilichokuwa ndani yake miaka ya 1993.
Aidha imeelezwa kuwa baada ya nyumba hiyo kuzama shimo hilo lilikuwa ni tishio kubwa kwa wakazi wa maeneo hayo ambalo lilikaa hadi mwaka 2004, lilipofukiwa kwa maroli na maroli ya vifusi vya mchanga na taka za kila aina.
Baada ya kutokea kwa tukio hilo wakazi walio wengi wa eneo hilo waliamua kuyahama makazi yao na wengine wakidiriki kuuza nyumba zao na kuhamia mahala pengine kama alivyofanya Spika wa Baraza la Wawakilishi, Pandu Ameir Kificho, ambaye aliamua kuuza nyumba yake iliyokuwa pembeni kabisa na shimo ilipozama nyumba hiyo na kuhama.
Eneo hili kwa sasa limekuwa salama ambapo vijana wa mtaa huo wanafanyia mazoezi ya Soka na hata wakazi wengine wakipita eneo hilo bila woga tofauti na siku za nyuma ambapo wengi walikuwa wameamua kuhamisha hata njia wakiogopa kupita karibu na eneo hilo kutokana na woga wa kuangalia shimo hilo lililokuwa likitisha kwa kina kirefu.

Hii ni njia ya kutoka barabara kubwa kuelekea eneo hilo ilipozama nyumba hiyo.

Hapa ndipo ilipozama nyumba hiyo ambapo kwa sasa hakuna hata anayethubutu kujenga hata banda la kuku.

Huu ni Msikiti uliokuwa pembeni mwa nyumba hiyo, ambao nao ulimegwa kipande cha ukuta na kuzama kama unavyoonekana ukuta uliojengwa baada ya eneo hilo kufukiwa.

Hii ndiyo nyumba iliyokuwa ya Spika wa Baraza la Wawakilishi, Pandu Ameir Kificho, ambayo aliiuza baada ya tukio hilo na kuahama.

Hii ni ofisi ya Askari Jamii iliyo katika mitaa hiyo.......

Mitaa ya eneo hilo.....

Mitaa ya eneo hilo.....

Hii ndiyo Barabara kubwa ya Jang'ombe.....Matarumbeta

No comments:
Post a Comment