Absalom Kibanda: Magufuli anasifiwa Tanzania wakati hana lolote
Akiwa katika kipindi cha TV cha Asubuhi Leo ya Channel Ten, Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Bw. Absalom Kibanda amesema Magufuli anasifika sana Tanzania kwa kujenga barabara kwa sababu watu hawajatoka nje ya nchi na kuona wenzetu wanavyojenga barabara. Akasema utamsifiaje Magufuli wakati foleni imejaa na inatisha? Akasema ni watu kuwa na fikra finyu na kutokujua kinachoendelea duniani.
Hii inanikumbusha maneno ya rafiki yangu mmoja anayefanya kazi Ivory Coast ambaye pia aliwahi kuniuliza hivi Tanzania wanamsifia kwa kujenga barabara zipi? Watu hawajaona wenzetu wanavyojenga barabara. Siyo unatumia trilioni kuikarabati Mandela road kwa lanes mbili zilezile na foleni ikabaki pale pale! Kinachomsaidia Magufuli ni ubabe tu but he is empty!.
Credit:Uspecial.
.jpg)
6 comments:
Mimi nadhani tatizo siyo magufulI,Mi naona tatizo ni idara za plannning.Waki-plan barabara za line mbili magufuli anazijenga japo siyo kwa standard inayotakiwa lakini zinajengwa.Ikiwa wataplan barabara za lane 6 kila upande na pesa ikawapo magufuli akasimamia kama anavyofanya sasa japo kwa ubabe zikajengwa mimi naona poa tu.
Angalia hata mipango miji,lamani zinatolewa bila kutengwa maeneo ya makaburi,utadhani tutaishi milele.hakuna mpangilio au usimamizi wa nani anajenga nini wapi,watendaji wamekaa maofisini hakuna mfuatiliaji ,sasa delivery itakujaje?
Kaka nakupongeza sana kwa kuliona hilo. Mimi naendesha kila siku inter state I-95 New York-Washington DC ambako kuna lanes nne kwenda na kurudi pamoja na emergence shoulders. Nimekuwa Tanzania mara kwa mara nikishangaa lane moja inatoka Dar kwenda Arusha na nyingine inarudi Arusha kwenda Dar. Na hiyo barabara iko tutani, kulia na kushoto ni ama mbuga, ama bonde. Sasa gari ya mbele yako ikisimama ghafla unafanyaje wakati kulia kwako kuna high speed incoming traffic? Matokeo yake ni vifo vya kila siku.
Ukweli kabisa.
huyu jamaa kweli ni kibanda siyo nyumba...akili yake finyu kuliko kawaida, huwezi kuishi kwa kujilinganisha na nyumba jirani coz siyo mashindano...tunajilinganisha kwa kuangalia tulikotoka na tulipo. Big up kwa Magufuli!
Yaani wee mdau hapo juu bwege kweli, maendeleo yanatokana na kuiga, kama hutaki kuiga basi utakuwa bado akili yako finyu..bongo magari yameongezeka barabara bado zilezile za enzi ya nyerere, Please. .
HUYU JAMAA CHA MAPOMBE KABISA LAZIMA TUIGE KWA WENZETU ILI TUPATE MAARIFA MAREKANI ILIKUWA KAMA TANZANIA MIAKA ILIYOPITA HADI LEO BADO WANAJENGA NA WANAIGA MIUNDO MBINU YA NCHI NYINGINE ZA ULAYA HUYU JAMAA SIJUI MAWAZO YAKE YAKO UKO NYUMA AU KATUMWA NA MAGUFULI KWANZA LAMI INAWEKA BAADA YA MIKA MITATU BONDE KILA KONA NA NYEMBAMBA HAKUNA MWISHO... PLANNING SCHEME IS POOR SUPERVISION IS HECTIC MUNGU
IBARIKI TANZANIA
Post a Comment