ANGALIA LIVE NEWS

Monday, January 6, 2014

KING CLASS KING CLASS MAWE AMTAKA CHEKA AACHE KUCHONGA NGENGA KING CLAA


BONDIA Ibrahimu CLass 'King Class Mawe' amekuja juu baada ya bondia Cosmas Cheka kupanda ulingoni siku ya Desemba 31 mwaka jana na kusema kwa Dar es salaam hana mpinzani na hakuna bondia
anaemuweza kumpiga kwa sasa na kumfanya bondia king class mawe kuja juu na kujibu mapigo kwa kusema ana kumbukumbu nzuri kwa kuwa tarehe moja January 2012 alichezea kichapo kutoka kwa Mohamed Matumla katika uwanja wa Jamhuri Stadium, Morogoro, Tanzania ambapo yeye ndipo anapotamba na katwangwa na Matumla ni wa Dar es salaam iweje leo aseme Dar hana mpinzani

kwa sasa nipo kwenye mazoezi makali nataka kugombania ubingwa wa taifa na Cosmas Cheka kwa kuwa promota wangu Mohamed Bawaziri nimeshamdokeza na kukubali kudhamini mpambano huo hivyo kwa sasa Cosmas akae mkao wa kupigwa tu kwani kwangu hana ujanja wananiita King Class Mawe ni mfalme wa mchezo wa masumbwi nchini ninaejiamini kuwa nikipambana nae atakuwa na uwezo wa kufika raundi ya nne kwa uwezo wake naujua hivyo hawezi kunibabaisha katika ulingo mimi ni zaidi yao hakuna asiyejua hilo alisema King Class Mawe ambaye amewatwanga mabondia mbalimbali akiwemo Said Mundi wa Tanga Patrick Kavako wa Morogoro na mabondia wakali kama vile Jonas Segu ,Amos Mwamakula ,Simba Watundulu na mabondia mbalimbali

Bondia huyo anayenolewa na jopo la Makocha linaloongozwa na Habibu Kinyogoli 'Masta' na kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' anae fundisha kwa njia ya digital

King Class Mawe aliongeza kwa kusema yeye anamsubili tu promota wake Mohamed Bawaziri apange siku ya mpambano huo ufanyika Dar es salaam au morogoro mana sitaki kuiacha nafasi hiyo ya kugombania ubingwa wa taifa hata kwa dakika moja kwani malengo yangu katika ngumi ni kufika mbali zaidi ya hapa nilipo alisema Class

No comments: