Mara baada ya kusaini mkataba huo wa kucheza raundi 10 za ubingwa wa Taifa kg,60 amesema atafanya mazoezi ya kutosha kuhakikisha ana msambalatisha mpinzani wake raundi za awali kwa kuwa alikuwa anachonga sana juu yake
mpambano huo uliodhaminiwa na Promota Maarufu nchini Jay Msangi utakuwa na msisimko wa aina yake kutokana na mabondia hawo kuwa gumzo katika ulimwengu wa masumbwi ndani na nje ya nchi ya tanzania
King Class aliongeza kwa kusema kuwa nipo fiti nimejiandaa na ninasubili tu kuvishwa ubingwa huo wa taifa kwani Cheka ana ujanja kwangu mbinu zake zote nimesha zikamata
King Class Mawe anae nolewa na jopo la makocha wanao ongozwa na Habibu Kinyogoli 'Masta' Rajabu Mhamila 'Super D' Kondo Nasoro
Bondio huyo amewashukulu wadau wa mchezo wa ngumi kwa kumuwezesha kuchaguliwa kuwa bondia bora wa mwaka katika uzito wake kwa kuwapita mabondia wengine wanne na yeye kuibuka kidedea katika kin'yan'gan'yiro hicho
No comments:
Post a Comment