Miongoni mwa wafanyabiashara waliozungumza ni pamoja na dada ambae aliongea kwa hisia kali sana mpaka machozi yakamtoka, anatokea Kilimanjaro na jina lake ni Neema Urassa ambae alizungumzia ujumla wa kodi za Tanzania akiorodhesha idadi ya kodi na namna ambavyo haziwasaidii kama wananchi.Mimi ni mmoja kati ya wanawake walioanza biashara wakiwa na umri mdogo mimi nmeanza biashara toka darasa la nne, naomba nitoe maoni yangu ambayo nimeona kama leo nisingeongea nisingelala, kodi ya Tanzania ukitaka kuichunguza iko kwenye makundi 8′
‘Kodi ya nyumba, Kodi ya duka, mzigo unaoleta unakatwa kodi, makadirio ya mwaka unakatwa kodi, bado mnatuambia na mashine……. hivi hizo kodi tunazolipa tutalipa ngapi jamani, unaweza kujikuta unalipa zaidi ya milioni 20 huku umechukua mkopo wa milioni 40 unajikuta umefanyia kazi mkopo na kodi’‘Angalia nchi ndogo kama dubai imeanza maendeleo juzi mwaka 1994, Dubai wanachajiwa kodi wafanyabiashara wote ndo maana ukienda kununua mzigo kila mfanyabiashara anakuuliza lete Risiti’
Hizi hapa chini ni dakika dakika 4 za huyu dada alivyoongea kwa uchungu kwenye mkutano wa wafanyabiashara uliofanyika Diamond Jubilee leo.
Katika risala iliyosomwa mbele ya Mgeni rasmi Mh Kigoda, wafanyabiashara hao walikumbushia waraka wao juu ya kero zao za mashine za kieletroniki za Efd, wakidai mfumo wa mashine hizo haufanyi kazi kwa ufanisi na kwamba unatoa nafasi za maafisa mbalimbali wa polisi wasiokuwa waaminifu kuingia na kuona hilo ni dili
No comments:
Post a Comment