Mama mzazi wa aliyekuwa Waziri wa Fedha na mbunge wa Kalenga
Consolatha Semgovano, mama mzazi wa aliyekuwa Waziri wa Fedha na mbunge wa Kalenga, mkoani Iringa, marehemu Dk.William Mngimwa, amevunja ukimya kuhusu kifo cha mwanaye akisema kuwa moyo wake unasononeka na umepoteza amani kwa sababu haoni ni nani katika familiya yake atakayeweza kuwa mbadala wake baada ya kuondoka kwa mwanawe.
Mama huyo anaeleza kuwa mzigo wa kulea watoto zaidi ya 200 ambao wanatoka katika familiya maskini za wakazi wa Jimbo la Kalenga hajui ni nani anaweza kujitoa kuubeba msalaba huo kwa sababu ni mtoto wake (Dk. Mgimwa) pekee mbaye alijali wanyonge na wasiojiweza.
“Hakuna anayeweza kujitoa kama William (Mgimwa) akaweza kuwapa watu chakula, akawasomesha watoto na kuwalipia ada. Inaniumiza na sijui wataishije baada ya sasa mlezi wao kufariki,” alisema Consolatha juzi alipozungumza na NIPASHE kabla ya mazishi ya marehemu Dk. Mgimwa nyumbani kwake katika kijiji cha Magunga.
Alisema Dk. Mngimwa ambaye ni mwanae wa kwanza kuzaliwa, ndiyealiyekuwa amabeba jukumu la kuwalea watoto wa ndugu zake ambao walifariki dunia na kwamba kifo chake kimeiachia familia mtihani mkubwa usiojibika.
Mara ya mwisho marehemu Dk. Mgimwa kufanya ziara ya kibunge katika jimbo hilo ilikuwa Mei 2013 wakati alipokwenda kutunisha mifuko ya vikundi vya wajasiriamali na hamasa.
Miongoni mwa ahadi zake kwa wakazi wa Kalenga ambazo hakuzitimiza na amemwachia wosia mwanawe wa kiume, Godfrey Mgimwa, ni pamoja na kugawa bati 1,200 alizoziacha kwa ajili ya ujenzi wa mabweni.

CHANZO: NIPASHE
No comments:
Post a Comment