ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, January 8, 2014

MANISPAA YA IRINGA YALIA NA UJENZI HOLELA

Meya wa Manispaa ya Iringa Aman Mwamwindi akizungumza na wanahabari leo kuhusu mambo mbali mbali yanayoendelea.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Iringa, Aman Mwamwindi akizungumza na wanahabari ofisini kwake. 
Ofisa habari wa manispaa ya Iringa Sima Bingileki akifuatilia kikao hicho.

HALMASHAURI ya Manispaaa ya Iringa imepiga marufuku ujenzi holela unaoendelea katika milima ndani ya mji wa Iringa .
Kauli hiyo imetolewa leo na mstahiki meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Amani Mwamwindi wakati akizungumza na wanahabari ofisini kwake.
Alisema kuwa udhaifu wa usimamizi wa sheria katika maeneo mbali mbali ndio umepelekea ujenzi holela kuendelea.
Hata hivyo alisema nyumba ambazo zinajengwa kiholela katika mji wa Iringa zitaendelea kuvunjwa iwapo itabainika kuwa zimejengwa kiholela.
Kuhusu uwekezaji alisema kuwa vipo viwanja kama vitatu ambavyo vinahitaji uwekezaji na hivyo kuwataka wananchi kujitokeza kuwekeza katika maeneo hayo.

CHANZO NI FRANCIS GODWIN BLOG

No comments: