Naibu Waziri wa Wizara ya Fedha, Mwigulu Nchemba, ambaye jana alikuwa miongozi mwa manaibu waziri walioapishwa na Rais Jakaya Kikwete kushika nyadhifa zao amewaambia watu wanaoponda uteuzi wake kuwa hana haja ya kubishana nao kwani hawamjui.
Katika maelezo yake, Mwigulu alisema anamshukuru Mheshimiwa Rais kwa kumwamini kuwa anaweza kumsaidia katika kusimamaia sera na mipango ya fedha nchini. Watu wasionifahamu wanadai mimi sina viwango vya kufanya kazi hii; naomba wafahamu kuwa mimi ni msomi mwenye shahada ya ya pili ya uchumi na hivi sasa niko katika masomo ya kupata shahada ya uzamivu.
Mwigulu aliendelea kusema “Kabla sijaingia kwenye siasa nilikuwa nafanya kazi katika Benki Kuu ya Tanzania kama mchumi. Ninakwenda Wizara ya Fedha kusimamia mambo manne ambayo ni uadilifu, ushirikiano, jitihada na huduma madhubuti ambazo zitatolewa kwa wakati mwafaka.
2 comments:
Wale Wale..
Hana jambo huyo, kapelekwa hapo kwa makusudi kwa vile uchaguzi mkuu unakuja hivi karibuni ili aandae mipango ya kukipatia Chama Tawala CCM fedha ya kampeni, kama ilivyokuwa kwa fedha za EPA kutoka Benki Kuu wakati ule. Unasikia Jamaa anatamba kwamba aliwahi kufanya kazi BOT! Amewekwa hapo kwa sababu ni mtu wa mipango haramu ya kuididimiza nchi na kuudhoofisha upinzani.JK na CCM hawana aibu wala woga, wanadhani wanainchi wote wamelala!!!!
Post a Comment