Jumuiya ya watanzania North Carolina ( UTNC )inaitisha mkutano mkuu utakaofanyika siku ya leo Jumamosi hii tarehe 25 mwezi huu, saa TISA mchana katika anuani ifuatayo 3400 BALFOUR WEST, DURHAM NC 27713.
Mkutano huo utawapatia wanajumuiya nafasi ya kubadilisha mawazo na kuamua kama kuna mabadiliko yoyote wayatakayo katika jumuiya ya UTNC na Uongozi wake.
Mkutano mkuu huo utatowa nafasi ya kuwasikiliza wana Jumuiya wote kwa njia ya kura za maoni kama wanataka uchaguzi mkuu wa chama ufanyike mwaka huu au mwaka ujao.
Sababu hasa ya kura hizo za maoni ni kwa kutokana na kushindikana kufanya Uchaguzi Mkuu mwaka jana.
Uongozi unawakaribisha wana jumuiya wote , ndugu jamaa na marafiki.


No comments:
Post a Comment