Moses raia wa Uganda anayeshiriki mapenzi ya jinsia moja
akitafuta hifadhi nchini Marekani
Rais wa Uganda, Yoweri Museveni amekataa kuidhinisha mswada
ambao ikiwa utaidhinishwa utatoa adhabu kali kwa watu wanaoshiriki mapenzi ya
jinsia moja.
Museveni amemuandikia spika wa bunge barua na kumkosoa kwa hatua ya kupitisha
mswada huo Disemba mwaka jana bila ya kuwa na idadi ya kutosha ya wabunge.
Aidha Rais amesema kuwa Watu wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja ni watu
wenye akili timamu na wanaweza kuokolewa kutokana na tabia hiyo.
Mswada huo unatoa adhabu kali kwa watu watakaopatikana na hatia ya kushiriki
mapenzi ya jinsia moja ikiwemo kufungwa jela na pia ni uhalifu kwa mtu yeyote
kukosa kuripoti visa vya mapenzi ya jinsia moja.
Mwandisi wa BBC mjini Kampala Cathrene Byaruhanga anasema kuwa mswada huo pia
unapendekeza kuadhibiwa kwa watu wanaozungumzia maisha ya wapenzi wa jinsia moja
bila ya kuwakashifu kwani wanaweza kufungwa jela.
Kwa mujibu wa gazeti la Monitor, Rais Museveni amesema kwamba mswada huo
ulishinikizwa zaidi kupitishwa na wabunge licha ya kuwashauri kusubiri hadi
serikali itakapoutathmini.
Rais anaelewa kwamba ikiwa atauidhinisha mswada huo na kuufanya sheria
kutakua na ukosoaji mkubwa kutoka kote hali inatakayochangia baadhi ya nchi za
kigeni kusitisha msaada kwa Uganda.
No comments:
Post a Comment