
Eusebio akibusu kiatu cha dhahabu baada ya kuibuka mfungaji bora wa Ulaya jijini Paris Ufaransa.
Mwanasoka wa zamani wa Ureno, Eusebio da Silva Ferreira, amefariki dunia akiwa na miaka 71 baada ya kusumbuliwa na ugonjwa wa moyo.
Alizaliwa nchini Msumbiji kabla ya kuhamia Lisbon, Ureno na kujiunga na timu ya Benfica.
Mwaka 1966, Eusebio alikuwa mfungaji bora wa Fainali za Kombe la Dunia kwa kufunga magoli tisa na kuisadia nchi yake kumaliza nafasi ya tatu.
Alifanikiwa kutwaa Kombe la Ulaya mwaka 1962 akiwa na Benfica.
Eusebio alikuwa mwanasoka bora wa Ulaya mwaka 1965. Katika mechi 745 alizocheza alifunga mabao 733.- GPL
No comments:
Post a Comment