ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, January 18, 2014

Papa Benedict aliwatimua makasisi 400

Vatican imekosolewa kwa kutowachukulia hatua makasisi wanaowadhulumu watoto
Takwimu zimejitokeza kuhusu idadi ya makasisi waliotimuliwa kufuatia madai ya kuwalawiti watoto.
Takwimu hizo zinaonyesha kwamba mnamo mwaka 2011 na 2012 aliyekuwa Papa Benedict aliwafuta kazi makasisi karibia 400.
Hii ina maana kwamba idadi ya makasisi waliopigwa marufuku kuhudumu katika miaka iliopita imeongezeka.
Idadi hiyo ilitolewa wakati wa maelezo yaliopewa maafisa wa Vatican wanaotarajiwa kufika mbele ya kamishna wa umoja wa mataifa mjini Geneva mapema juma lijalo.
Hadi kufikia sasa Vatican imeripoti idadi ya visa vya unyanyasaji wa kimapenzi pekee.
Kanisa katoliki limetuhumiwa kwa kuficha vitendo vya unyanyasaji wa kimapenzi vinavyotekelezwa na viongozi wa dini, kwa kuwahamisha makasisi hadi parokia nyengine na kukosa kuwafikisha kwa mamlaka.

4 comments:

Anonymous said...

ndo maana mkuu wa dini anatakiwa awe anaoa siyo kukaa kisela sela ukika hivyo shetani na mapepo machafu yatakufuata utende mambo maovu na kujiharibia

na cha pili hivi kwa nini wanawandama ukatoliki kwanini tujiulize katika madhehebu yote ya kiikiristo ukatoliki ulikuwa ni bora na imara tujiulize ni kwa nini wanauandama kuna kitu hapa mimi nishakijua je wewe unakijua tafadhalini tuchangiye

Anonymous said...

mimi pia nishakijua uislamu ndio dini ya kweli

Anonymous said...

Mdau WA pili kila dini ina ukweli wake amini unajokijua wewe. Kama unasema uislamu ni dini ya kweli amini hivyo. Na mkritu atasema hivyo hivyo we need to respect each others. Kina mtu ni mdhabi uwe mwislam au mkristu sote tu wakosefu. Tunahitaji huruma ya mungu. No one is perfect

Anonymous said...

Mdau WA pili kila dini ina ukweli wake amini unajokijua wewe. Kama unasema uislamu ni dini ya kweli amini hivyo. Na mkritu atasema hivyo hivyo we need to respect each others. Kina mtu ni mdhabi uwe mwislam au mkristu sote tu wakosefu. Tunahitaji huruma ya mungu. No one is perfect