ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, January 23, 2014

Profesa Lipumba ‘awasha moto’ wa Katiba Zanzibar

Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba
Zanzibar. Chama cha Wananchi (CUF) kimesema CCM kama wana ubavu wawafukuze mawaziri wakuu wastaafu; Jaji Joseph Warioba na Dk Salim Ahmed Salim na mwanasiasa mkongwe, Joseph Butiku kwa kwenda kinyume na sera yao ya serikali mbili kwa kupendekeza Serikali tatu.
Msimamo huo ulitolewa na Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba alipozindua kampeni za uchaguzi mdogo za chama hicho Jimbo la Kiembesamaki, juzi.
Profesa Lipumba alisema haikuwa mwafaka kumfukuza uanachama aliyekuwa Mwakilishiw a chama hicho, Mansoor Yussuf Himid kwa madai ya kwenda kinyume na maadili na kukiuka sera ya CCM kwa kufungamana na wazo la kutaka muungano wa serikali tatu.
Alisema Mansoor alitakiwa kuenziwa na CCM siyo kuadhiriwa kama ilivyotokea, kutokana na mchango mkubwa aliotoa hayati baba yake kupigania Mapinduzi ya Zanzibar mwaka 1964.
“Mansoor ni mtoto wa mwasisi wa Mapinduzi ya Zanzibar, kama mmemfukuza kwa kutaka Serikali tatu, je mna ubavu wa kuwafukuza kina Dk Salim, Butiku na Warioba, hawa wote wanataka Serikali tatu badala ya mbili,” alisema.
Alisema msimamo uliobebwa na CCM utawamaliza wanaCCM wote, wanaotaka mabadiliko ya mfumo katika Muungano hasa kwa kuzingatia Wazanzibari wengi wanataka Zanzibar yenye mamlaka kamili.
Tangu kutoka kwa rasimu ya pili ya Katiba Mpya, wanasiasa wakongwe na viongozi wa juu wa CCM wamekuwa wakipinga pendekezo la kuwa na Muungano wa Serikali tatu na kwamba, wazo hilo linaweza kuvuna Muungano na kuyumbisha taifa.
Vyama vya upinzani vinaonekana kuafiki mapendekezo ya Serikali tatu.
Pia, alisema katika uchaguzi huo mdogo, anatakiwa kupatikana mtu mwenye uwezo wa kutetea maslahi ya Zanzibar hasa kwa kuzingatia mwakilishi huyo atakuwa kati ya wabunge wa Bunge la Katiba.
huku akiwataka wananchi wa Kiembesamaki kumchagua mgombea wa CUF Abdulmalik Haji Jecha aweze kuwatewtea.
Alisema baada ya kufungua mkutano huo atafanya pirikapirika za kukutana na Rais Jakaya Kikwete ili kuhakikisha uchaguzi huo unakuwa huru na wa haki huku akiitaka SMZ kutoruhusu vyombo vyake vya ulinzi kuingilia shughuli za uchaguzi.
Kwa uapnde awake mgombea wa chama hicho Jecha,aliwataka wananchi wa Kiembesamaki kutambua umuhimu wa uchaguzi huo na kuwataka kiti hicho kukipelekea CUF na si kwingineko.
“Uchaguzi huu hatumwi mtoto,mimi ndiye nitakayevaa viatu vya Mansoor,tayari safari imeanza ya kisasa ili kulitwaa jimbo hilo na kukiacha solemba”Alisema Jecha.
Uchaguzi mdogo wa Kiembesamaki unafanyika kufuatia kufukuwa uanachama wa CCM kwa Mansoor mabpo sasa wagombea sita wa vyama vya CCM, ADC, CUF, TADEA, Chadema na SAU wanachuana katika kinyng’anyiro hicho ambapo kura zitapigwa Februari pili mwaka huu.
Mwananchi

No comments: