Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazungumzo na Rais Goodluck Jonathan wa Nigeria wakati viongozi hao wawili walipokutana na kufanya mazungumzo Alhamisi, Januari 23, 2014, kwenye Hoteli ya Intercontinental, Davos, Uswisi, ambako walikuwa wakihudhuria Mkutano wa Mwaka huu wa Taasisi ya Uchumi Duniani –WEF.
PICHA NA IKULU
THE
UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE
OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
|
Telephone: 255-22-2114512,
2116898
Fax:
255-22-2113425
|
|
PRESIDENT’S
OFFICE,
THE STATE HOUSE,
P.O.
BOX 9120,
DAR
ES SALAAM.
Tanzania.
|
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais
Kikwete aalikwa Nigeria na Rais Jonathan
Rais wa Nigeria Mheshimiwa Goodluck
Jonathan amemwalika Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya
Mrisho Kikwete kuhudhuria Mkutano wa Taasisi ya Uchumi Duniani Afrika (WEF-Africa) unaofanyika katika mji mkuu
wa Nigeria wa Abuja mwezi Mei mwaka huu.
Rais Jonathan ametoa mwaliko huo kwa
Rais Kikwete wakati viongozi hao wawili walipokutana na kufanya mazungumzo leo,
Alhamisi, Januari 23, 2014, kwenye Hoteli ya Intercontinental, Davos, Uswisi,
ambako viongozi hao wanahudhuria wa Mkutano wa Mwaka huu wa Taasisi ya Uchumi
Duniani –WEF.
Rais Kikwete amekubali mwaliko huo wa
kuhudhuria Mkutano huo uliopangwa kufanyika Mei 7-9 mwaka huu mjini Abuja,
Nigeria.
Mkutano huo kati ya viongozi hao
wawili umehudhuriwa na Mawaziri wa Nigeria wa Mambo ya Nje na Fedha na Uchumi.
Nigeria inakuwa nchi ya nne katika
Afrika kuandaa mkutano huo. Kwa miaka mingi, mkutano huo wa WEF-Africa ulikuwa
unafanyika Cape Town, Afrika Kusini mpaka Tanzania ilipofanikiwa kuwa nchi ya
kwanza ya Afrika nje ya Afrika Kusini kuandaa Mkutano huo mwaka 2010.
Tokea wakati huo, Ethiopia imeandaa
mkutano huo na sasa Nigeria.
Imetolewa
na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR
ES SALAAM.
23 January, 2014



No comments:
Post a Comment