Heri ya Mwaka Mpya 2014 Mungu azidi kukubariki katika Mwaka 2014
* Karibuni wote kwenye Ibada za Kila Mwezi kwa Mwaka 2014*
**Karibu uanze siku njema kwa NENO la Mungu kila siku kwenye ukurasa wa Facebook na Website**
***Karibu Kwa Mafundisho ya NENO Kila Ijumaa ya kwanza ya Mwezi kwa njia ya Simu***
*Tembelea Website ya Ibada ya Kiswahili - www.iykcolumbus.org kwa Matukio ya Mwaka 2014*
www.iykcolumbus.org
www.iykcolumbus.org
Facebook: Ibada ya Kiswahili - Columbus, Ohio
UJUMBE MAALUM 2014: Ibada ya Kiswahili inakuhimiza kushiriki kwenye Jumuiya zetu kwa Ukamilifu. Tuwe chachu ya mabadiliko ya kimaendeleo. Tuige mema. Mapungufu tuyatatue haraka na kwa kutumia Busara.
NENO LA LEO: Wafilipi 4:13, Nayaweza
mambo yote katika yeye anitiaye nguvu.
TAFAKARI: Kuna mambo tulipanga kufanya katika
mwaka huu uliyoisha, lakini kwa sababu moja au nyingine tulishindwa. Kuna ndoto
na malengo mengi hayakuwa vile kama tulivyo tarajia na kwa namna moja au
nyingine tumevunjika moyo. Mwaka mpya unaanza, inatupasa kujifunza kutokana na
makosa ya mwaka uliopita na kumwamini Mungu ndani ya mwaka huu kuwa tutayaweza
yote kupitia yeye atutiaye nguvu. Yeye Bwana Yesu atatutia nguvu ya kufanya
yote ambayo tupasayo kufanya katika mwaka huu mpya. Atatuwezesha kufanya yale
kwa nguvu na upeo wetu hatutaweza, unapoanza mwaka weka imani yako kwake. Mfanye
yeye awe nguvu zako katika mwaka huu mpya chini ya uongozi wa Roho wake
Mtakatifu, kila jambo na mpango litakuwa sawa sawa na mapenzi yake katika
maisha yako.
SALA: Mungu wangu, naomba unitie nguvu ya
kufanya mambo yote ulinikusudia nifanye katika mwaka huu mpya. Nipate kufanya
mambo yote sawa sawa na mpango wako ili Jina lako lipate kutuzwa kupitia miasha
yangu. Kwa Jina la Yesu, Amina. (c) IYK_NENO

No comments:
Post a Comment