ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, January 29, 2014

SHOGA, UMEMLETA MWENYEWE NDANI, UNAKIMBIA NINI?


JAMANI hamjambo naona viroho vinawadunda baada ya kuufunua ukurasa huu na kujiuliza leo kombora linaangukia kwa nani? Jamani narudia sipo kwa ajili ya kuwarusha roho bali mtajirusha wenyewe kutokana na tabia zenu mbaya.

Nia yangu ni kumuona mwanamke mwenzangu mambo ya kike hayampiti kando.
Jamani kuna mambo mengine yanasikitisha, hivi kwa nini umuogope mwanamke mwenzio mwenye viungo kama wewe?

Juzi nilikutana na mtoto wa shoga yangu akiwa anatoka sokoni, katika mazungumzo yetu si unajua mimi mtu wa utani. Mwenzenu sijui kukasirika kijinga, mtoto wa kike niliumbwa siku Mungu akitabasamu nami nikawa na umbile la tabasamu siyo wewe uliumbwa Mungu akiwa amechoka kila wakati uso kama ndimu unacheka hujulikani umenuna hujulikani.

Si kwamba nazungumza wenye sura mbaya, hakuuu! bali wenye sura zilizokosa tabasamu, siwezi kumuhukumu mtu kwa maumbile kwa vile mimi sijawahi kuumba. Ila nazungumza na tabia za watu, Mungu kawaumba na sura nzuri lakini imeharibika kwa kukunja uso na kupinda midomo kila wakati.

Hebu tuachane na hayo tuendelee na yetu, basi katika kutaniana si ndiyo aliponieleza kaamua kurudi kwao baada ya mumewe kuoa mwanamke mwingine. Nilimuuliza kipi kikubwa kilichomuondoa kwa mumewe ikiwa dini yake inamruhusu. Alinipa jibu la kitoto ambalo lipo katika vichwa vya wanawake wengi.

Eti ameondoka kwa vile hawezi kushea mwanaume na mwanamke mwenzake. Jibu lake nililinifanya nimwangalie chini mpaka juu mpaka akashtuka na kuniuliza kulikoni kumuangalia vile! Nilimweleza na yeye akae chini ili nimweleze aache woga na kushindwa kujiamini.

Jamani ni kweli wanawake tupo kama mdudu wa sikio tusiotaka mshirika, lakini kutokana na hali ya sasa hivi kuwa na wako wa peke yako kazi. Afadhali dini zingine zinaruhusu mpaka wake wanne, lakini dini zilizokataa tunaona jinsi gani viongozi wao wanavyoingia kwenye kashfa ya kuwa na wanawake wengi tofauti na muongozo wa dini yake.

Siyo kwamba nahalalisha lakini ukweli ndiyo ulivyo asilimilia kubwa ya nyumba zetu waume zetu wana wanawake zaidi ya mmoja. Wengine tunawakamata na wasichana wetu wa kazi imefikia hata kuwapa ujauzito.

Hii yote inatokana pengine na udhaifu wetu ndani ya ndoa zetu kwani wengi baada ya kuolewa hujisahau na kuamini ukiisha olewa ndiyo umemaliza kila kitu. Tumekuwa hatuzithamini ndoa zetu kwa kuamini baada ya kuolewa hakuna kingine zaidi kwa mumeo kama umemvulia nguo ya ndani ndiyo baaasi.

Tunasahau mwanaume anatakiwa kutunzwa kama mtoto kwani wewe ndiye kila kitu kwake siyo kasoro zitolewe na mwanamke wa pembeni. Pengine mumeo hakuwa na wazo la kuongeza mwanamke mwingine, lakini mwanamke mwenzako ameona upungufu wako na kuufanyia kazi ndiyo yaliyomfanya mumeo aingie kichwakichwa baada ya kunasa aliendelea kumpa vitu adimu ambavyo kwako hapati. Ili afaidi vizuri anamuoa kabisa kuepuka kula kwa kujificha.

Unaletewa mke mwenza unakimbia kumbe sababu ni wewe. Kaingia ndani hutakiwi kukimbia jirekebishe, pigana kuhakikisha unairudisha namba moja yako.
Nina imani nimesomeka vizuri, basi kwa leo inatosha tukutane wiki ijayo,

Ni mimi Anti Nasra Shangingi Mstaafu.

GPL

1 comment:

Anonymous said...

Watch your mouth girl muumba hana sifa ya kuchoka