
Akizungumza na NIPASHE kisiwani hapa jana, Tambwe alisema Logarusic ameifanya timu yao icheze soka la kuvutia na kwa ushirikiano mkubwa.
"Logarusic ana uwezo mkubwa wa kufundisha mpira. Kwa sasa tunacheza mpira mzuri na tunacheza kitimu tofauti na mfumo wa makocha waliokuwapo kabla yake (Kibadeni na aliyekuwa msaidizi wake, Jamhuri Kihwelo 'Julio')," alisema Tambwe.
"Kabla ya kuja Logarusic, tulikuwa tunacheza kila mchezaji kuonyesha juhudi binafsi lakini sasa timu yote inashirikiana. Naamini tutafanya vizuri zaidi chini yake," alisema zaidi mshambuliaji huyo wa timu ya Taifa ya Burundi.
Hata hivyo, licha ya uzuri wa Logarusic, Tambwe, mfungaji bora wa Kombe la Kagame mwaka jana na kinara wa mabao katika msimamo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara hajafunga hata bao moja katika mechi tano za mashindano yanayomalizika leo kisiwani hapa ya Kombe la Mapinduzi.
CHANZO: NIPASHE
No comments:
Post a Comment