ANGALIA LIVE NEWS

Friday, January 10, 2014

TASWIRA YA KESI YA ALIYEKUWA MKURUGENZI WA SHIRIKA LA VIWANGO TANZANIA (TBS)


Aliyekuwa Mkurugenzi wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Charles Ekerege (kulia) na familia yake akitoka katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam jana kusikiliza mwenendo wa kesi yake ya matumizi mabaya ya madaraka kwa kutoa asilimia 50 ya punguzo la tozo ya utawala kwa Kampuni mbili na kulisababishia TBS hasara ya Dola 42,543 za Kimarekani.
Aliyekuwa Mkurugenzi wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Charles Ekerege na binti yake wakiondoka katika viwanja vya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam jana kusikiliza mwenendo wa kesi yake ya matumizi mabaya ya madaraka kwa kutoa asilimia 50 ya punguzo la tozo ya utawala kwa Kampuni mbili na kulisababishia TBS hasara ya Dola 42,543 za Kimarekani. 
MASHAHIDI wa Jamhuri katika kesi inayomkabili aliyekuwa Mkurugenzi wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Charles Ekerege (pichani) ya matumizi mabaya ya madaraka kwa kutoa asilimia 50 ya punguzo la tozo ya utawala kwa Kampuni mbili na kulisababishia TBS hasara ya Dola 42,543 za Kimarekani, wamedai kwa nyakati tofauti kwamba mshtakiwa alitoa msamaha huo bila kibali cha Baraza la Utendaji (kwa sasa Bodi ya Wakurugenzi).

No comments: