ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, January 23, 2014

Tikitaka za Mzee Reginald Mengi: Anamiliki share katika makampuni yenye vitalu vya mafuta na gesi.

Reginald Mengi
Na Mwandishi Wetu
Katika Mjadala uliofungwa hivi karibuni na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dr Jakaya Mrisho Kikwete juu ya suala la Uzawa kwenye utafutaji na uzalishaji wa mafuta na gesi hapa nchini. Mjadala huo ambao kwa kiasi kikubwa ulibebwa na pande mbili yaani upande wa Serikali chini ya Waziri wa Nishati na Madini Mheshimiwa Prof Sospeter Muhongo na upande wa sekta binafsi chini Mzee Reginald Mengi. Tamati ya Mjadala huo ambapo Rais Jakaya Kikwete aliufunga kwa kubainisha kuwa inatosha kwa makampuni ya Serikali kuwawakilisha watanzania katika mchakato wa ushirikishwaji wao katika utafutaji na uvunaji kwa kuwa gharama za mchakato huo ni wa gharama kubwa ambao watanzania wazalendo walio wengi hawana uwezo wa kumudu.

Hitimisho hilo ambalo limekuwa mwiba kwa Mwenyekiti wa Sekta Bnafsi Nchini Bwana Reginald Mengi kwa kuwa si tu ni kiongozi wa sekta binafsi nchini bali pia ni mtu mwenye maslahi ya moja kwa moja na biashara ya utafutaji, uchimbaji na uvunaji wa rasilimali za madini, mafuta na gesi. Hitimisho hilo ni mwiba kwa kuwa hoja aliyoisimamia imeonekana kushindwa mbele ya jamhuri.

Lakini taarifa iliyopatikana punde ambayo ni sahihi, na ambayo imeendelea kuonyesha sarakasi za Mzee Mengi katika suala hilo ni kwamba; Mzee Mengi ni mbia mwenye shares kwa asilimia 3.3 katika kampuni ya watanzania inayofahamika kwa Jina la SWALA ambayo ina blocks 2 za kutafuta mafuta na gesi huko Kilombero na Pangani. Kampuni hiyo ambayo inaongozwa na Mwenyekiti wa Bodi Bwana E. Massawe na Mkurugenzi wake Bwana B Mramba.

Taarifa hizi zinaudhihirishia Umma kuwa Mzee Mengi anapigania hoja hii kwa maslahi binafsi na pili inaonyesha ni kwa namna gani amekuwa ni mtu asiyeridhika pamoja na kumiliki sehemu kubwa ya ardhi yenye madini na hata kufanikiwa kupata nafasi katika vitalu vya gesi na mafuta ameendelea kumshutumu Waziri wa Nishati na Madini kwa tuhuma za kutengeneza na hata kumkashifu kuwa ni kiongozi wa Hovyo ambaye anafaa kupelekwa milembe kuangaliwa akili yake.

Kwanza ni makosa na kinyume cha Sheria na Kanuni za Madini kwa mtu mmoja kujilimbikizia eneo kiasi hicho, na makosa mengine ni kuwa yapo maeneo ambayo hajayaendeleza na sheria inaweka bayana kuwa baada ya miaka 2 mtu asiyeendeleza eneo lake anatakiwa kunyang'anywa asilimia 50 ya eneo hilo, na usipoliendeleza lililobaki katika miaka 2 ijayo unapoteza eneo zima, hivyo kwa maeneo ambayo Mzee Mengi anayamiliki na hajayaendeleza ni vyema sheria ikafuata mkondo wake na anyang'anywe maeneo hayo.

Kauli za Mzee Mengi na mtindo wa Shutuma zake kwa Waziri ulionesha ni kwa kiasi gani Mzee Huyu amekosa busara na hekima katika kufuatilia na kufikisha hoja zake, lakini utumiaji wa vyombo vya habari anavovimiliki na vile ambavyo ana ushawishi navyo kuwashutumu mahasimu wake na hata kuwakatisha tamaa watanzania juu ya mipango na mikakati ya maendeleo ya Serikali yao ni makosa mengine ya msingi katika tasnia ya habari na kwake kama mmiliki, makosa ambayo ni ya kukusudia na yenye kutoa taswira mbaya mbele ya jamii.

Umefika wakati wa watanzania kuwaelewa watu hawa ambao katika macho ya jamii wanajipambanua kama wapigania haki, wakweli na wenye huruma hali ya kuwa uhalisia wa ndani ni watu wabadhirifu, walafi na walanguzi wasiotosheka.

6 comments:

Anonymous said...

sidhani kama Mtanzania kujipambanua na kuwa tajiri kwa rasilimali yetu ya asili ni ulafi, uzandiki au chochote

Mengi ni mtanzania aliyeona fursa, na rais wetu alisisitiza sana wazawa kuchukua fursa, naridhika sana kuona akina mengi wanakamata fursa, wanajenga tanzania, wanaoa tanzania, wanaishi tanzania, wananunua petroli tanzania, wanalipa luku tanzania, wanaenda ngorongoro, serengeti, mikumi nk... tanzania, wanaenda haja pia tanzania

nakwazika na makaratasi na nadharia za makusanyo ya wageni in the name of mega investment, hatuna haraka ya kuchimba kila kitu, ni bora mengi kuchimba mdogomdogo tukaiga kuliko mkoloni kubutua mashimo na machimbo yote mara moja na kutuacha na papers na tax declaration forms huku hata mishahara wanalipa HSMC, standard na barclays ya canada, usa, australia nk.

mwizi wa nyumbani anakula na nduguze, mwinzi wa mataifa hupeleka kwao

ZIMWI LIKUJUALO, LAHIKULI LIKAKWISHA

Anonymous said...

Mengi's selfishness is behind all this rhetoric that's carefully calculated to mislead wananchi wa Tanzania. Anachotaka ni kujenga mazingira ya kujinufaisha yeye binafsi. Akishamilikishwa vitalu vya kutosha baadaye ataanza kuvilangua kwa wawekezaji wenye mitaji na uwezo wa kweli. Mengi ni msanii wa siku nyingi. ....Mmeshawahi kuona wapi Mengi katoa msaada bila kuwepo kamera za waandishi wa habari? Never!!! He'll never quietly mail anyone in need a check or make a wire transfer to a needy group without holding a press conference. Hiyo sio misaada. Ni usanii at best au biashara ya kununua umaarufu (elevation of his social status).

Joy Mbaga said...

Tuna penda kumona kiongozi mwema kwa manafaa ya nchi yetu Asante mr Mengi kwa juhudi zako .Joyce .USA.

Anonymous said...

mbona kama vile sijamuelewa huyo anayejiita MWANDISHI WETU.,,,kosa la Mengi hapo nilipi?
nilichoelewa mimi nikua Mengi anahitaji watanzania wapewe nafasi kubwa kuliko wageni na hakujizungumzia yeye pekee hata kama alikua na nia ya ubinafsi.
OMBI
Acha kuupotosha Umma. Kama Rais ameshafunga mjadala basi ww usianzishe yako juu ya taarifa iliyofungwa,,,,,,AHSANTE

Anonymous said...

Baadhi ya comment za hao hapo juu ni kutaka kuona kama Mengi hana makosa ya kisheria, Tanzania ina sheria zake ambazo zinatakiwa kufuatiliwa na kama Mengi ni mkosaji kama wakosaji wengine atachukuliwa hatua kisheria kwa makosa yake.

inavyofanya sasa serikali kua na mikataba wawekezaji wa kigeni ndivyo pia' hata Mengi atakavyo fanya, biashara zake, hazitaiishia kwa waTanzania pekee bila kuwa na wawekezaji wa kigeni.

cha msingi anachatakiwa ni kuonyesha kama mfanya biashara mweye-ubora na mfano wa kuigwa, serekali inajua kwa kina uzuri na uoza wa baadhi ya Embezzld"

mdau holland.

Anonymous said...

Acheni majungu kama ana uwezo wa kuwekeza si mumuachie sidhani kama kwenye nchi za magharibi wanateteaga wageni kushinda wazawa hata kama anatetea kwa maslahi binafsi muachieni kwani ana haki kama mtanzania asipowekeza kwao atawekeza wapi.Go Mengi wengine wana wivu tu