ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, January 23, 2014

Tuhimizane tupendekeze Watanzania wanaojituma kuokoa mama na vichanga wapewe TUZO ya kimataifa

.

Kama ambavyo nimeahidi ntakuwa nawarudieni tena na tena na tena kwa ajili ya kupeana habari mbali mbali zihusuzo uhai wa akinamama na watoto wachanga nchini mwetu.

Leo nina mawili makuu. 1--Tuzo 2--Kielelezo yaani factsheet.

Kuna TUZO maalum kwa wadau waliojituma zaidi ili kuokoa mama zetu na vichanga. Yaweza kuwa mtu mmoja mmoja au taasisi na vikundi. Ni TUZO ya Afrika kwa hiyo shime tupendekeze majina ili Watanzania wang'are. kwenye tuzo ya MSambazeni ujumbe na watu wasome link hii kwa taarifa zaidi http://bit.ly/1dy8i5h

Vile vile Mama Ye! tunajipanga tuwe tunatoa kijarika kila mwezi ili tutaarifiane vizuri masuala haya. 

Natanguliza shukrani kwa ushirikiano na moyo wako wa kutumia taaluma na nafasi yako kwenye kampeni ya kuwaokoa wajawazito na vichanga wa Tanzania.

Wako katika harakati

Chiku Lweno-Aboud
Communications & Advocacy Coordinator

Evidence for Action (E4A)
164C Msasani Beach, 
P.O. Box 13731, Dar es Salaam
www.mamaye.or.tz/sw      

No comments: