Rais wa Jumuiya ya Watanzania DMV Bwn. Iddi Sandaly akiongea kwenye kisomo cha mpendwa wetu Zainab Buzohera kulichofanyika jana Jumanne Jan 7, 2013 katika ukumbi wa mirage uliopo Langeley Park, Maryland na kuhudhuriwa na Watanzania wa DMV na majimbo mengine kama New York, New Jersey, Massachusetts, Georgia, Ohio, Pennsylvania na kwingineko. Mwili utaondoka leo Jumatano Jan 8, 2014 na kufika Ijumaa Dar ses Salaam, Tanzania siku ya Ijumaa na utaambatana na dada ya marehemu Jasmine Bernett na Mume wa marehemu Dullah wakiwemo Watanzania kadhaa hapa Maryland na majimbo mengine.
Mwambata wa Jeshi katika Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani na Canada, Colonel Adolph Mutta akiongea kwa niaba ya Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani na Mexico, Mhe. Liberata Mulamula ambaye yupo Tanzania.
Wafiwa mdogo wa marehemu Ngalu Buzohera (wapili toka kushoto baibui nyeusi) na Dada wa narehemu Jasmine Bernett (watatu toka kushoto) wakifuatilia kisomo cha mpendwa wao kilichofanyika jana Jumanne Jan 7, 2014 Langeley Park Maryland.
Juu na chini ni Jopo la Watanzania wakiwemo maafisa Ubalozi wakiongoza kisomo cha kumuombea mpendwa wao kilichofanyika jana Jumanne jan 7, 2014 Langley Park, Maryland.
Juu na chini umati wa Watanzania wa DMV na majimbo mengine waliohudhuria kisomo cha mpendwa wetu Zainab Buzohera kilichofanyika Jumanne Jan 7, 2014 Langeley Park, Maryland katika ukumbi wa Mirage.
kwa picha zaidi bofya soma zaidi
17 comments:
Kwenye msiba ni mahala pa huzuni, lakini kwenye picha hizi watu wengi wanaonekana wana furaha, kweli haileti maana nzuri. RIP ndugu yetu.
Mungu Aibariki DMV wanaushirikiano.
watu karibu wote wamepiga picha wame-smile kasoro mdogo mtu. watanzania hapo ndo napochoka. watu hamuonyeshi sura ya huzuni hata kidogo what a shame! wengine wamevaa tight jeans na vichwa wazi. i know ilikuwa siku ya kazi lakini mtu angeweza kubeba kanga au mtandio kwa mkoba.
Huyo aliyesema kuwa msiba ni uzuni kasema kweli....visomo vingi watu wanapelekwa kula tu nakupiga picha hili waonekane that's all. Kazi ya kupiga picha kuonyesha nani alikuwepo ni kazi ya mpiga picha...acheni kimbelembele...hasa akina baba...
We nae embu tuondolee ushuzi wako humu sasa ulitaka watu walie twenty four seven? wivu tu umeona wenzio wamependeza kwenye picha ndo wajitia kusema kwenye msiba ni mahala pa huzuni mxiiiii. Watu wanalia then maisha yanaendelea. wewe anonymous wa kwanza hapo juu get a life
sasa wote wakiwa na huzuni nani atawafariji?
Luke weka comment niliyomjibu huyo anony wa kwanza. acha kuchagua comments za kuziweka humu usilete ufala wako hapa, watu lazima waambiwe ukweli
mdau wa hapo juu unakosea msiba ni sherehe ya mwisho ya marehemu ya hapa duniani, lakini kutokana na ubinadamu huwa hatuwezi kusheherekea. kwahiyo hao unawaona wanacheka sio kama hawana huzuni bali wanafarijiana. Zay B you wil always be missed. Rest in Peace Sister
jamani huyo anon wa kwanza hajaandika ushuzi bali ni opinion yake binafsi. wewe anon wa 3 kulikuwa na ulazima gani wa kutukana na mipasho juu? RIP Zay
wewe unayesema ati watu hawna uzuni unakili mukichwa kweli ! sasa ulitaka tufanye nini?tulie tuuuu! kama tungekua hatuna uzuni nae hata mchango usingetimia kwa masaa matatu,, unapiga makelele wakati mchango wenyewe umetoa $20 , tutolee upuuzi wako hapa.
Mmmh wabongo kwa kupenda mizozo na matusi, ka sijui ndio ma box yanstiwa watu wszimu..tuelimikeni jamani...
kweli msiba ni uzuni sana ila ni kweli kwenye msiba si kila wakati watu wataonekana wameuzunika lzm kuna kufurahi,ndio maana tumeambiwa kuna wakati wakucheka na kuna wakati wakulia.
mi nilifiwa na mama yangu kweli ni maumivu sana asikwambie mtu kufiwa na mtu wako wa karibu inavyouma,hata hapo huyo mdogo mtu simpatii picha ni maswali gani anayojiuliza kichwani ambayo hayapatii jibu,kwanza unakuwa kama unaona kama si kweli kama vile unaota....lkn katika machungu hayo hayo kuna wakati mtu unajikuta mnaongea na wenzako nakucheka ndio inavyokuwa.
Watu wametoka kwenye background tofauti, hizo kanga kuna wenzangu nasisi hatuzijui. Ulimwengu umejazwa na watu wa kiaina. Tuvumiliane tofauti, alafu kulia hata mimi ninapicha nimepigia kwenye msiba wa mama mzazi tunacheka na kuvaa vizuri. Marehemu alikuwa mtu wa furaha na vicheko atakuwa na furaha kuona anaagwa kivicheko...badilika its a new selfie world and things has change for cheese and show.
Hata Mandela alipokufa walikuwa wanaimba na kucheza sana. Lakini kuna wakati mnaongea na kucheka. Mtu anaweza kuonyesha sura ya uzuni Au ya kulia lakini isimaanishe kitu chochote. Kila mtu ana huzunika. Kwa hiyo Kama mtu hajalia sio ndio Hana huzuni.
Jamani! kabla haujapost fikiria kwanza ,kama wewe Mtanzani wa ukweli kule bongo siku ya msiba kuna zile jadi watu wanataniana na kucheka na kuakashifiana,, hii ni mila na desturi yetu,,ni moja ya kuwawaliwaza wafiwa,, mimi mwenyewe siku ya msiba nilimwambia mume wa marehem Dullahyahoo 'tukimaliza alambee twende tukacheze kamali hizi pesa' alicheka sana akasahau hata kulia,fikiria kabla haujaandika kitu.
jamaa uliyesema watu hawana uzuni umechemsha.
Post a Comment