ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, January 22, 2014

WAKAAZI WA NEW YORK WAPATA ADHA YA SNOW NA BARIDI KALI

People walk past the art instalation 'Red Cube' by Isamu Noguchi during a snow storm that is moving through the Northeast on January 21, 2014 in New York City. Along with dropping arctic tempertures the storm is expected to bring three to five inches by nightfall, with another four to six inches falling overnight.
Watu wakitembea karibu na sanamu ya umbo inayojulikana kama 'Red Cube'  wakati tufani ya theluji ilpokua inaanza kuanguka New York "Jiji lisilolala" siku ya Jumanne January 21, 2014 na kusababisha nyuzi joto kushuka na kusababisha shule kufungwa yakiwemo maeneo mengi yakazi zikiwemo huduma za mabenki kwa ajili ya usalama wa wafanyakazi wao kuelekea nyumbani mapema kabla hali haijakuwa mbaya. Theluji iliyoanguka ilikuwa kati ya inchi 5 mpaka 10. 
A couple walks through a snow storm that is moving through the Northeast on January 21, 2014 in New York City. Along with dropping arctic tempertures the storm is expected to bring three to five inches by nightfall, with another four to six inches falling overnight.
Wawili wakitembea kwenye theluji iliyoanza kuanguka mitaa ya jiji lisilolala, New York siku ya Jumanne January 21, 2014, Theluji hiyo iliendelea kuanguka kwenye majimbo mengine yaliyopo ukanda huu wa kaskazini mashariki ya Marekani na kuleta baridi kali iliyosababisha theluji kuwa barafu iliyoleta adha kubwa kwa waendesha vyombo vya moto na viwanja vingi vya usafiri wa anga kusitisha safari.
A man walks through a snow storm that is moving through the Northeast on January 21, 2014 in New York City. Along with dropping arctic tempertures the storm is expected to bring three to five inches by nightfall, with another four to six inches falling overnight.
Mdau akikatiza mitaa ya New York huku akipata kikombe cha kahawa kuongeza joto mwilini siku ya Jumanne January 21, 2014 wakati theluji ilipokua ikianza kuanguka kwenye jiji hilo lisilolala.
A man shovels snow during a snow storm that is moving through the Northeast on January 21, 2014 in New York City. Along with dropping arctic tempertures the storm is expected to bring three to five inches by nightfall, with another four to six inches falling overnight.
Mdau akijaribu kukwangua theluji iliyokuwa ikiendelea kuanguka kwenye jiji la New York siku ya Jumanne January 21, 2014 na kusababisha nyuzi joto kushuka na kuleta bariki kali siku ya leo Jumatano.
The Statue Of Liberty is obscured during a snowstorm that is moving through the Northeast on January 21, 2014 in New York City. Along with dropping arctic tempertures the storm is expected to bring three to five inches by nightfall, with another four to six inches falling overnight.
Sanamu ya Liberty  ikiwa haionekani kutokana na tufani hiyo ya theluji iliyoanguka kwenye mji huo wa New York siku ya Jumanne January 21, 2014. Theluji ilianza kuanguka kuanzia saa 4 asubuhi mpaka usiku wa manane na kuleta baridi kali.
People walk along Wall Street during a snowstorm that is moving through the Northeast on January 21, 2014 in New York City. Along with dropping arctic tempertures the storm is expected to bring three to five inches by nightfall, with another four to six inches falling overnight.
Watu wakitembea mtaa wa Wall wa New York wakati wa tufani hiyo ya theluji ilpokuwa ikiendelea kuanguka siku ya Jumanne January 21, 2014.
A delivery man bikes through the snow in Union Square during a snowstorm on January 21, 2014 in New York City. Areas of the Northeast are predicted to receive up to a foot of snow in what may be the biggest snowfall of the season so far.
Mpiga box akiwa na wakati mgumu wakujaribu kugawa vidonge kwenye tufani ya theluji iliyoanguka siku ya Jumanne January 21, 2014 na kuleta baridi kali iliyowapa wakati mgumu wakaazi wa mji huo wa jiji lisilolala. Picha kwa hisani ya Zimbio

No comments: