Kanye West mwanamuziki wa Hip Hop wa Marekani huenda akawa nyuma ya nondo baada ya kumpiga jamaa aliyekuwa akibugudhi mchumba wake Kim Kardashian Jembo hiyo ilikua ikijaribu kuwaita waandishi wa habari wampige picha Kim Kardashian jambo ambalo halikufurahisha mrembo huyo na badala yake akaenda kumwambia Kanye West nae bila ajizi alimfuata jamaa huyo ofisini kwake na kumalizana naye

wakati huo huo inasemekana Kim Kardashian alimtumia ujumbe Beyonce wa kumtaka awe mpambe wake kwenye harusi yake na Kanye West lakini habari Vijimambo ilizozipata ni kwamba Beyonce kamtolea nje mrembo huyo.

Jana Jumanne Jan 14, 2014 timu ya kikapu ya Miami Heat yenye maskanii yao Florida ilitinga jengo jeupe kwa Rais Barack Obama kupeleka kombe lao la ubingwa wa Kikapu walilonyakua mwaka jana na kumzawadia jezi namba 44.
Ciera katika picha ya pamoja na mchumba wake kwenye BET Award
Mwanamuziki Ciera mwenye maskani yake Atlanta Georgia ametangaza kwamba sasa hivi na mama kijacho habari hizo zilienea kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii ya Marekani na Radio mbalimbali za hapa. Ciera ambaye anatoka kimahaba na mwanamuziki wa kufokafoka anayeitwa Future aliyemvishwa pete ya uchumba hivi karibuni.
No comments:
Post a Comment