ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, January 25, 2014

Yanga kuonyesha vitu vya Uturuki leo

Kocha msaidizi wa Yanga,Charles Mkwasa.
Mabingwa watetezi wa ligi kuu ya Vodacom, Yanga Afrika leo inashuka kwenye uwanja wa Taifa kuwaonyesha mashabiki kile walichokifuata Ututuruki walipokwenda kuweka kambi ya wiki mbili kujiandaa na mzunguko wa pili wa ligi kuu unaoanza leo kwenye viwanja tofauti.

Yanga ambayo iliwasili jana asubuhi ikitokea Antalya nchibni Uturuki leo itataka kuonyesha kuwa ushindi wa magoli 5-1 walioupata kwenye mchezo wa mzunguko wa kwanza wa ligi kuu dhidi ya 'Watoto hao wa Ilala' haukuwa wa kubahatisha.


Kwa mujibu wa ratiba ilitolewa na Shirikisho la soka nchini (TFF) inaonyesha kuwa leo kutakuwa na mechi nne katika viwanja vinne tofauti.

Kwenye uwanja wa Azam Comlex, wenyeji Azam FC watawakaribisha Mtibwa Sugar, wakati Coastal Union iliyorejea juzi ikitokea Oman itapambana na JKT Orjoro huku Kagera Sugar watacheza na Mbeya City kwenye uwanja uliofanyiwa ukarabati wa Kaitaba, Bukoba mkoani Kagera.

Pamoja na michezo hiyo, macho na masikio ya mashabiki wa soka yatakuwa kwenye uwanja wa Taifa wakati vijana wa Jangwani watakapotaka kuonyesha kuwa awakwenda Uturuki kutalii.

Kocha msaidizi wa Yanga, Charles Mkwasa alisema hana wasi wasi na kikosi chake kutokana maandalizi yao na kwamba wamejipanga vya kutosha kuhakikisha wanaonyesha nini walikwenda kufanya nchini Uturuki.

Aidha, alisema kuwa pamoja na kuzuiwa kucheza kwa mshambuliaji wao mpya, Emannuel Okwi, bado anaimani na wachezaji wengine kwa kuwa wanauwezo mkubwa wa kuiletea ushindi Yanga.

"Sina wasiwasi na timu yangu.., maandalizi ya Uturuki yametusaidia sana, pamoja na kuwa hatutakuwa na Okwi mimi binafsi badio ninaimani na wachezaji wengine kwa sbabu wanauwezo mkubwa," alisema Mkwasa.

"Tuna washambuliaji wengi ambao ndio hao hao wameifanya Yanga kuongoza ligi kwenye mzunguko wa kwanza hivyo kukosekana jkwa Okwi sioni kama kutazuia Yanga kufanya vizuri," aliongezea kusema Mkwasa.

Alisema kuwa timu ikiwa nchini Uturuki walifanyia marekebisho mapungufu yote ambayo yalionekana wakati timu hikiwa nchini.

Mchezo wa leo ni wa kwanza kwa makocha Mkwasa na mkuu wake Hans van der Pluijm

ambao wamechukua mikoba ya Ernest Brandts na Fred Felix 'Minziro' waliyoingoza timu hiyo kwenye mzunguko wa kwanza kabla yakutupiwa virago Desemba mwaka jana.

Kwa upande wake, Kocha wa Ashanti, Abdallah Kibadeni, alisema kuwa hana hofu na Yanga kwa kuwa anaimani na kikosi chake na kama watacheza kwa kufuata maelekezo yake wataibuka na ushindi leo.

"Kila timu imefanya maandalizi kulingana na uwezo wake, sina hofu na Yanga kwa sababu naijua, nimeandaa timu yangu kwa ajili ya kuzikabili timu zote kwenye ligi ikiwemo Yanga," alisema Kibadeni.

Alisema hawahofii Yanga pamoja na kuwa ni mabingwa na pia wametoka nje ya nchi, anachoangalia ni kuibuka na ushindi kwenye mechi ya leo ambayo ni ya kwanza kwake tokea asaini mkataba wa kuinoa timu hiyo mzunguko huu wa pili akitokea Simba.
 
CHANZO: NIPASHE

No comments: