Hapa ilikuwa ni pata shika ambapo dada huyo amewekwa kati huku vijana wa eneo hilo wakiwa wanapiga kelele huku wakimvua nguo na kumfanyia vitendo visivyo vya kibinadamu
Anaeonekana kwa mbali ni mdada ambaye alijitolea kwenda kumsaidia dada huyo ambae alikuwa amevaa kanguo kafupi ka nusu utupu akikatiza maeneo kituo cha basi cha mwenge usiku huu
Hapa akiwa amevuliwa nguo na baadhi ya kina mama kumsaidia na kumwingiza katika gari moja wapo ili kumsitili
Umati wa watu ukiwa umeongezeka na kuzingira basi hilo la abiria na kudai ashushwe ili waweze kumchapa na viboko kwa kitendo cha kuwadhalilisha akina dada wengine
Angalizo: Hatukuweza kuweka picha za binti huyo akiwa mtupu kulingana na maadili.
Picha na Dar es salaam yetu
6 comments:
Joto hasira wananchi mpunguze kujichukulia sheria mikononi kwani akivaa nguo fupi inawahusu nini? mnaacha kwenda kuwapiga wabunge wanaokula pesa zenu za kodi na kuwafanya maisha yenu yawe magumu mnashikilia kudhalilisha mwanamke acheni hasira zisizo na msingi
Huku ni kukosa ustaarabu,hatuja fikia hatua ya kuvuana nguo hadharani.Jamani where is this Country heading to? backward!
Sasa kama amevaa nguo fupi nyinyi ni nani wakumchukulia hatua? Tena mnavua na kuudhalilisha mwili wake! Dola iko wapi? Hivi kama ni Dada yako kweli ungethubutu kumgusa? Panahitajika upelelezi hapa na wahusika wote wafikishwe mbele ya sheria..ni kifungu kipi cha sheria kinachohalalisha ubakwaji hadharani kisa kuvaa nguo fupi? Kama nyie ni wema mbona hamkumfunika na nguo ndefu? Mamlaka zetu zinaangalia mwanamke anavyodhalilishwa kijinsia na wahuni barabarani:(
" Annually on 8 March, thousands of events are held throughout the world to inspire women and celebrate achievements." Yet, in this century, African women, and Tanzanian women in general are not being respected, they are not given equal justice, and they are not given the social economic benefits same like men.
Women, like men, they have the freedom to pursuit good life, freedom to pursuit pleasure, and freedom pursuit hierarchical needs. In this essence, the ministry of home affairs and security of government of Tanzania has failed on protecting the own people from the endangerment. It is time for a change- educating the men to respect women of all ages and social classes.
http://www.laxengineeredsolutions.com/Maxon-32731-p/32731.htm
Dr. Temba
Hii inaonesha Tanzania kama nchi inachukuliaje mwanake...kila mwanaume asiye rijali anaona ana haki ya kudhalilisha anayemuona hathaminiwi ili tu ajisikie ana uanaume hata ukiwa feki...
dr Temba I salute you sir with all my brain you are such a brave man to come out and write such a knowledgeable thoughts I wish some Tanzania man can think and act like you.
mungu akubariki sana dr Temba.
with all due respect I salute you sir for what you wrote;it shows how much you value women and especial Tanzania women.
NY,
Post a Comment