Katibu
Mtendaji Bodi ya Filamu Tanzania, Bi. Joyce Fissoo (kulia) akieleza
jambo wakati alipokutana na mtangazaji wa kipindi cha Amplifaya cha
Clouds FM, Bwana. Pancras Mayala (kushoto) leo katika ofisi za Bodi
jijini Dar es Salaam.
Na. Benedict Liwenga-Maelezo
Bodi
ya Filamu Nchini imekiri ongezeko la uzingatiaji wa Sheria ya Filamu na
Kanuni zake unaofanywa na watengenezaji na wasambazji wa filamu wa ndani
na nje ya nchi. Aidha imethibisha kuwa uwasilishaji wa filamu Bodi
umeongezeka kwa kiwango cha kuridhisha baada ya wengi wa wadau kuitikia
wito wa kuwasilisha kazi zao ili ziweze kukaguliwa na kupewa madaraja
stahiki.
Vile
vile Bodi imefafanua kuwa filamu na muziki iliyo katika video
isiyofungiwa kwa kukosa maadili na zinazoendelea kurushwa ama kuonyeshwa
bila kuzuiwa haimaaninishi ni halali isipokuwa zinapaswa kuwasilishwa
Bodi kwa mujibu wa Sheria na Kanuni kabla ya kwenda kwa walaji.
Hayo
yamesemwa leo na Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Tanzania, Bi. Joyce
Fissoo wakati alipokuwa akifanya mahojiano na Clouds Media Group ofisi
kwake jijini Dar Bi. Fissoo amesema kuwa Bodi ya Filamu ilianzishwa kwa
mujibu wa Sheria ya Filamu na Michezo ya Kuigiza namba 4 ya mwaka 1976
Sheria ambayo ilitanguliwa na Sheria ya Picha za Sinema ya mwaka 1930
jambo linalodhihirisha ukongwe wa tasnia ya filamu nchini. Bodi inafanya
kazi zake kwa kujielekeza katika kusimamia Sheria ya hiyo na Kanuni
zake .
Akijibu
swali toka kwa mtangazaji wa kipindi cha Amplifaya cha Clouds FM, Bwana
Pancras Mayala lililotaka kujua filamu ngapi zilizofungiwa na Bodi ya
Filamu na sababu za kufungiwa kwa filamu hizo, Bi. Fissoo amesema kuwa
mpaka sasa ofisi yake imepoke na kushughulikia jumla ya kazi zipatazo
1059 kutanzia 2011 hadi Januari 2014 ikiwa ni kwa maana ya majina.
“Mwaka
2011 mpaka sasa tumepokea na kushughulikia filamu 1059 ikiwa ni kwa
maana ya majina, lakini ukienda kwa maana ya Part 1 na Part 2 maana yake
ni jumla ya filamu 2118 ambapo kati ya hizo filamu 123 sawa na asilimia
5.8 zilielekzwa kufanyiwa marekebisho na filamu 7 sawa asilimia 0.33
hazikuruhusiwa kati ya mwaka 2011 hadi juni 2013 ambazo ni za ndani na
za nje 2.4 hazikuruhusiwa.
Aidha
kati ya Julai 2013 hadi 2014 jumla 570 zilipokelewa zikiwemo filamu 263
zilizokuwa zimeshaingia sokoni na kati ya hzo filamu 16 zilielekezwa
kufanyiwa marekebisho. Tayari filamu zilizoelekezwa kufanyiwa marekesho
14 zimekwisha wasilishwa na kupewa kibali na filamu mbili za MV Spice na
Nimekubali Kuolewa hatuajapokea marekebsho. Hakuna filamu iliyofungiwa
kati ya julai 2013hadi Januari 2014”. Alisema Bi. Fissoo.
Aliwapongeza
wadau wa filamu kwa kupunguza kwa kiasi kikubwa filamu zisizoendana na
maadili na kusisitiza umuhimu wa kuzingatia ubora na viwango. Kwa upande
wake mtangazaji wa Clouds Media, Bwana Mayala alitaka kujua ni vigezo
gani vinavyotumika katika kuzuia filamu zisiende kwa walaji ambao ni
watazamaji, Bi. Fissoo alifafanua kuwa Bodi ya Filamu inazuia filamu kwa
mujibu wa sheria na vipo vipengele mbalimbali vitumikavyo katika
kufanya zoezi hilo aidha alimpitisha mtangazaji huyo aktika vifungu
hivyo vya sharia na kanuni .
vile
vile alieleza kuwa kabla ya kufikia hatua hiyo maneneo yote
yanayoshauriwa kurekebishwa au kuondoshwa hupitiwa kwa pamoja kati ya
Bodi na wenye kazi na kufikia muafaka. Katika eneo hilo tumeendelea
kupata ushirikiano mkubwa sana.
Aidha,
Bi. Fissoo amewaasa wadau mbalimbali wa filamu Tanzania kushirikiana
kwa pamoja katika kutekeleza mambo yaliyoelekezwa kwa mujibu wa sheria,
na kwa wasanii amewasisitizia kuwasilisha miswada ya kazi zao ili iweze
kupitiwa na Bodi na baadae filamu iwezwe kutengenezwa. Alisisitiza kuwa
ofisi za Bodi ziko wazi kwa wadau wote na wakati wowote wanapohitaji
ufafanuzi wanakaribishwa kwa bodi kwa ajili ya kuwahudumia wananchi wote
chanzo:HAPA
No comments:
Post a Comment