Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiwa pamoja na Mke wa
Waziri Mkuu Mama Tunu Pinda wakijumuika pamoja katika kulisakata rumba
kwenye tafrija ya kukaribishwa kwa Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba
Mjini Dodoma.
Waziri
Mkuu Mh. Mizengo Pinda akiwa na Mke wa Mbunge wa Mpendae Mama Tamima
Turky wakionyesha manjonjo yao katika mduara wa tafrija ya kuwakaribisha
wabunge wa Bunge Maalum la Katiba wa CCM.
Raha
iliyoje kwa Mke wa Waziri Mkuu Mama Tunu Pinda Kushoto, Mke wa Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Suleiman Iddi na Mbunge wa Viti
Maalum Chek chake Pemba Mh. Faida Mohd Bakari wakati wakiliskata rumba
kwenye tafrija ya kukaribishwa wabunge wa Bunge Maalum la Katiba wa
Chama cha Mapinduzi.
Waziri
Mkuu wa Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Mizengo Pinda
akimpongeza Mkurugenzi wa Mlimani Grand Mark Bwana Fredy Sam kwa ubunifu
wake wa kujenga Ukumbi wa Kisasa ndani ya Manispaa ya Mji wa Dodoma. Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ.
**********************************
Waziri
Mkuu wa Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Mizengo
Kayanda Piter Pinda amesema majaribio yote ya changamoto zilizotokea
ndani ya miaka 50 ya Muungano wa Tanzania lazima yaendelee kulinda na
kudumisha amani na utulivu uliopo Nchini.
Mh.
Pinda alisema hayo katika tafrija maalum ya kuwakaribisha Wawakilishi
wa Baraza la Wawakilishi, Wabunge wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa
Tanzania pamoja na Wajumbe wa Bunge Maalum ya Katiba wa Chama cha
Mapinduzi wanaokutana Mjini Dodoma kujiandaa kujadili Katiba Mpya ya
Jamuhuri ya Muungano.
Tafrija
hiyo iliyoandaliwa na Ofisi ya Faragha ya Makamu wa Pili wa Rais wa
Zanzibar kwa kushirikiana na baadhi ya wahisani wakiwemo Wabunge
ilifanyika katika Ukumbi wa Kilimani Grand Mark uliopo pembezoni mwa
Magharibi ya Mji wa Dodoma.
Waziri
Mkuu Mizengo Pinda alisema Dunia imeshuhudia muungano wa Mataifa kadhaa
iliyoundwa katika mifumo tofauti hasa ule wa Shirikisho ambayo hatma
yake ilikuwa ni fupi na bila ya mafanikio.
Alieleza
kwamba waumini na wasimamizi wa Muungano wa Tanzania ambao bado
unaendelea kuwa pekee na wa mfano Barani Afrika katika Kipindi cha
miaka 50 iliyopita wanapaswa kusimamia Umoja, Mshikamano na Upendo huo
uliopo miongoni mwa Wananchi.
Naye
kwa upande wake Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi
akitoa nasaha zake katika tafrija hiyo alisisitiza kwamba Wabunge wa
Bunge Maalum la Katiba ndio watetezi halisi wa Wananchi wote Nchini
Tanzania.
Balozi
Seif alisema matarajio ya Jamii ya Wananchi wa Tanzania Bara na
Zanzibar ni kuendelea kuishi katika maisha ya furaha yaliyojaa
matumaini ya kujengeka kwa hatma yao ya baadaye hasa katika kujikwamua
kiuchumi.
Alifahamisha
kwamba licha ya wananchi walio wengi kutoa maoni yao katika vikao na
mikutano ya Tume ya Katiba Mpya ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ya
kueleza mfumo wa Katiba wanayoihitaji lakini bado jukumu la kuboresha
mfumo huo hivi sasa limo ndani ya mikono ya Waheshimiwa Wabunge wa Bunge
hilo Maalum la Katiba.
Alitahadharisha
kuepukwa kwa ushabiki na kisiasa miongoni mwa Wabunge hao wa Bunge
Maalum la Katiba ambao unaweza kuharibu lengo la Taifa lililokusudiwa la
kupatikana kwa Katiba Mpya ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliwapongeza Wabunge wa Bunge hilo Maalum
la Katiba kwa kupata fursa hiyo adhimu na kuwaomba kuitumia vyema ili
kiu ya Wananachi waliyonayo iwewe kuwafikia.
Mapema
Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Zanzibar Nd. Vuai Ali Vuai
alisema uwepo wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ndio uliosababisha
Umoja, Upendo na Mshikamano miongoni mwa Wananchi wote wa Tanzania Bara
na Zanzi bar.
Nd.
Vuai alisema Heshima hii ambayo imekuwa tunu kwa Mataifa mbali mbali
Duniani hasa ndani ya Bara la Afrika inafaa kulindwa na kudumishwa kwa
faida ya jamii yote.
4 comments:
Watanzania ni wazuri sana when it comes to sherehe, hafla etc.Sasa hawa wajumbe wanapongezwa kwa lipi walilolifanya so far.
1.wameteuliwa kuwepo hapo walipo.hapakuwa na mashindano yoyote.
2.Kupongezwa kungeleta maana kama wangefanya baada ya kutupatia katiba bora.
"Mungu ibariki Tanzania" kazi tunayo.
Well said @post#1
Wanapongezwa kwa kula kodi yetu, wabongo tumelala! Nchi inaliwa na wajanja. They have been there for more than a week and have actually done zero work or nothing. Iko kazi. Did we really need this Bunge Katiba? Jamani - anything they come with should be rejected.
Be careful of your comments. Otherwise will be denied dual citizenship...lol
Post a Comment