ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, February 22, 2014

HARAMBEE YA KUKAMATWA KWA KENYATA

Kenyatta akiwa na mkewe Juliana siku alipofunga ndoa mwezi march mwaka jana

Ndugu zangu Watanzania kesho Jumamosi Feb 22, 2014 kuanzia saa 10 jioni (4pm) kutafanyika harambee ya kusaidia kumtoa ndugu yetu, kaka yetu, Mtanzania mwenzetu na Baba mzazi wa Barakat Kenyatta Mayanga aliyekamatwa na uhamisji siku ya Jumanne Feb 18, 2014 asubuhi  kazini kwake. Familia imeishaongea na mwanasheria wa uhamiaji na pesa tasilimu zinazphitajika ni $5000/.

Tunaomba msaada wako wa haraka utakaowezesha kumtoa ndugu yetu, Mtanzania mwenzetu, Baba wa mtoto wa miaka 8 anayejitaji mapenzi na malezi ya baba yake ambaye kila giza liingiapo anakaa karibu na mlango akimsubili baba yake aliyeenda kazini tangia Jumanne mpaka leo Ijumaa hajarudi nyumbani.

Harambee itafanyikia 
6200 Ager Rd, 
Hyattsville, MD 20782

Kwa marafiki wa Kenyata waliopo mbali na DMV wanaweza kusaidia kupitia  052001633 acc#446019426077. BANK OF AMERIKA Jina la Acc ni MWINYIKHERI SEIF MKWAVI.

Kwa maelezo zaidi wasiliana na
Mwinyikheri Mkwavi 240 603 3274
Juliana Morris 781 354 2983
Jabir Jongo 240 604 0574

Kufika kwako ndio kutafanikisha kumtoa mwenzetu 
ASANTE NA TUNATANGULIZA SHUKURSNI.

11 comments:

Anonymous said...

nasikia kuna watanzania wengine wamekamatwa huko DMV kuhusiana na home health care agencies na medicaid fraud, tujuzeni

Anonymous said...

Tuko pamoja. Asante kwa kutujulisha

Anonymous said...

Kaka Harambee ni ya Kenyatta mbona mnamuanika dada wa watu bila sababu. Kwa kweli sidhani ni fair kuweka picha kama hii. Kenyatta anajulikana vya kutosha na hii picha ni kuingilia privacy yake na ni sawa na kumuanika wazi bila sababu. Luke please naomba hii iondolewe jamani

Mdau wa kila siku vijimambo.

Anonymous said...

Masha allah wamependeza kweli kweli, Tuwekee na picha ya mwanawe ili tuweze kumsaidia kwa haraka na wingi zaidi
Asante
MDAU

Anonymous said...

Anonymous #1, asante kwa kutupa mwanga kuwa kuna ndugu zetu ambao wameshikwa katika operesheni ya fraud hapa DMV. Itakuwa ni vyema kama viongozi wa jumuiya wataitisha kikao cha dharura ili tuone jinsi tunavyoweza kuwasaidia. Ndugu Luke, jaribu kutangaza hilo kwenye blogu yako. Hamna haja ya kuficha maana hao ni ndugu zetu who just made bad choices in life, but can be helped if we stick together.

Anonymous said...

KAKA KENYATTA KUMBE HATA WEWE MAKARATASI OUT? MAJANGA , KARIBU MOROGORO TUNAKUSUBIRI KWA HAMU!

SASA MUDA WOTE HUU ULIKUWA UNAFANYA NINI HUKO. NASIKIA WABONGO WOTE HUKO HAMNA MAKARATASI SASA KWA NINI MNATAKA URAIA PACHA KUMBE HATA WA HUKO KWA OBAMA BADO, YAANI KAZI KWELI KWELI. LAKINI MUNGU AKUSAIDIE AKUEPUSHE NA HILI .

Anonymous said...

wewe mwandishi hapo juu ukitaka pesa za watu ukubali kuanikwa unaomba pesa unakuwa huna choices nyingi tena? huo.ndio ukweli.kikubwa toa pesa acha kutafuta makosa

Anonymous said...

Mdau hapo juu unataka kujuzwa kitu gani? Hujui kusoma au kusikiliza habari? Unafiki umekujaa tu.

Anonymous said...

huyu ndio yule wa kutoka ugiriki na anashiriki vijiwe ughaibuni?naomba majibu tafadhali kaka luke, mimi mfatiliaji mkubwa wa vijimambo pamoja na kijiwe
mdau michigan

Anonymous said...

NDIYO YEYE KWENYE KIJIWE CHA UGHAIBUNI

Anonymous said...

luka mbona ubenia comment yangu ya lniliyoweka link ya kuwanyamazisha wanafiki?