ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, February 23, 2014

JESHI LA POLISI MKOA WA IRINGA LAPIGA MARUFUKU WANANCHI KUHUDHURIA KWENYE MIKUTANO YA KAMPENI NA MARUNGU,MAPANGA


index
Na Datus Boniface, Jeshi la Polisi Iringa
JESHI la Polisi mkoa wa Iringa limepiga marufuku kwa Mwananchi kuhudhuria mikutano ya kampeni wakiwa na marungu na mapanga hasa wakati huu wa kampeni za kuwania kiti cha Ubunge Jimbo la Kalenga.Aidha, limewataka kuacha mara moja wataka wamiliki wa Malori kubeba wafuasi na wapenzi wa vyama vya siasa kwa lengo la kuwapeleka katika mikutano ya kampeni. 
 Akizungumza jana na waandishi wa habari, Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Iringa Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP), Peter Kakamba alisema Jeshi la Polisi halitavumilia mtu atakayevunja sheria katika kipindi hiki cha Kampeni na uchaguzi.“Uzoefu tuliopata katika chaguzi ndogo za Udiwani wa Kata za Nduli, Ibumu na Ukumbi ziligubikwa na vitendo vinavyoashiria uvunjifu wa amani ikiwemo wafuasi wa vyama mbalimbali kushambuliana pamoja na kutembea na marungu na mapanga”alisema 
Aliongeza kwamba, katika chaguzi hizo yalitokea matukio mbalimbali yakiwemo ya kuingiliana ratiba za kampeni na viwanja na pia kujichukulia sheria mkononi kwa kuwapiga watu bila sababu za msingi au kwa hisia kwamba ni wapinzani wa vyama vyao

No comments: