MABAO
mawili ya Jordan Henderson na mawili ya Daniel Sturridge yameipa
Liverpool ushindi wa 4-3 dhidi ya Swansea katika mchezo mgumu wa Ligi
Kuu ya England jioni ya leo Uwanja wa Anfield.
Kikosi cha Brendan Rodgers kimeendelea kuwanyatia vinara wa ligi, Chelsea sasa wakizidiwa kwa pointi nne tu.
Mabao
ya Swansea yalifungwa na Jonjo Shelvey moja na mawili Wilfried Bony.
Liverpool inatimiza pointi 56 baada ya kucheza mechi 27, ikiendelea
kutulia nafasi ya nne, nyuma ya Manchester City pointi 57 mechi mechi
26, Arsenal pointi 59 mechi 27 na Chelsea pointi 60 mechi 27.
Henderson akipongezwa na Glen Johnson baada ya kuifungia Liverpool bao la ushindi |
Bao la ushindi: Kiungo wa Liverpool, Jordan Henderson alifunga bao la nne kwa Liverpool ikishinda 4-3
Sturridge akimzunguka kipa wa Swansea, Michel Vorm kabla ya kufunga leo
No comments:
Post a Comment