Rais wa kwanza Tanzania
Mwl. Julius K. Nyerere
Yamekuwepo malumbano na mada nyingi kuhusu uraia pacha na jinsi ilivyo muhimu kuwa na uraia pacha kwa Watanzania wanaoishi nje ya nchi, na hapa namaanisha siyo ughaibuni tu hata wale waishio nchi jirani zinazotuzunguka.
Pamoja na mada zote nzuri naomba kwa ruksa yenu turudi kwenye sheria yenyewe ya uraia Tanzania kama inavyojulikana kama (Tanzania citizenship Act no 6 1995). Katika mada yangu hii naomba tujikite hasa kwenye aina ya uraia unaotambuliwa na sheria hii pamoja na lengo la kutunga sheria hii iliyofanyiwa marekebisho mara kwa mara kulingana na mahitaji ya muda huo na mwanzo baada ya uhuru iliitwa Tanganyika Citizenship Ordinance 1961 na Zanzibar Citizen Decree.
Mwaka 1964 ndipo Tanzania Citizenship Act ilipotungwa na kupewa no. 6. Mabadiriko haya yalikuwa yanafanyika kwa nia ya kuwabana walowezi, wahaini. pamoja na kuhakikisha usalama wa taifa changa la Tanzania kwa kipindi kile. Ndani ya sheria hii inatamka kuwa Tanzania itakuwa na uraia wa aina nne kama ifuatavyo: uraia wa kuzaliwa; uraia wa kuandikishwa; uraia tajinisi nauraia wa kurithi.
Kwa muda huu naomba tujikite kwenye uraia wa kuzaliwa na maana halisi ya uraia huu. Hii ni haki ya kwanza ya msingi ya kila binadamu aipatayo mara tu anapozaliwa na hii haki inaambana na ulinzi na ustawi wa huyu binadamu . Haki hii unaipata hajali wazazi wako ni kabila gani, rangi gani au dini gani. Tunaposema huyu ni mtanzania tuna maana gani? Ni mtu yeyote mwenye sifa moja wapo hapo juu aidha kazaliwa, kaandikishwa, karithi au katajinisiwa. Sasa turudi kwenye kiini. Uraia pacha hapa ndipo mkanganyiko unapoanzIa, nini maana yake? Huyu ni mtu mwenye uraia wake wa asili na amepewa au anatarajia kupata uraia wa nchi nyingine kwa kujiandikisha Kwenye nchi anayoishi. Siku zote bila kuelewa historia ya wapi ulikotoka, uliko na unapotarajia kuelekea ni vigumu kutambua nia na madhumuni ya kila jambo .
Kuhahama kwa binadamu kulikuwepo tangu enzi za Adam na Hawa. Kuhama huku ilikuwa ni kujitafutia riziki pamoja na maisha bora kwa binadamu wenyewe wanyama, ndege na hata wadudu hufanya tendo hili ila kuhama hama huku hakumfanyi mtu aache asili yake. Mifano ya wazi kabisa ndani ya nchi yetu tunaona wachaga, wahaya wanyakyusa, wamakonde na makabila mengine mengi yalivyohamia Dar es salaam lakini hatujasikia mchaga aliyehamia Dar ameacha kuwa mchaga anaendelea na asili yake. Siyo rahisi kumnyanganya asili yake eti kwa sababu tu anakaa kwa wazalamo na wadengereko . Vivo hivyo . Mkude akiwa mmarekani hataacha kuwa mlugulu hata muta akiitwa smith hataacha kuwa mhaya.
Katika sheria ya uraia iliyotajwa hapo juu imekuwa ikiwanyima haki hii ya msingi kabisa Watanzania waliokwenda nchi za inje kuchuma na kutafuta marisho mabichi ili kuwasaidia ndugu zao na Taifa kwa ujumla. Ieleweke wazi kuwa kondoo kuzaliwa zizi moja na mbuzi habadiriki kuwa mbuzi anabaki kuwa kondoo. Watanzania tunaoishi nje tunataka hii haki yetu ya msingi iwekwe kwenye sheria mama ya Katiba na itamke wazi kabisa kuwa mtanzania wa kuzaliwa yeyote na kizazi chake hawapotezi uraia wa Tanzania. Kwamba, hakutakuwa na mamlaka yeyote ndani na nje ya mipaka ya Tanzania ya kumvua uraia na haki zote. Manufaa ya kuwa na uraia pacha yamegawanyika katika nyanja zote za maisha kama mada zilizotangulia zinavoelezea.
Imeandaliwa na Emil Muta, Mwenyekiti wa Watanzania wa Washington-Seattle katika jitihada za Jumuiya za Watanzania za Marekani na DICOTA katika kuelimisha umma kuhusu suala la uraia pacha.
Imeandikwa na Emil Muta ambaye ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Watanzania ya Washington Seattle na Dakta Anicetus Temba Mweka Hazina msaidizi wa Jumuiya ya Watanzania New York.
Imeandikwa na Emil Muta ambaye ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Watanzania ya Washington Seattle na Dakta Anicetus Temba Mweka Hazina msaidizi wa Jumuiya ya Watanzania New York.
2 comments:
Ningependa kuongezea,ktk inchi za EAC ni Tanzania pekee ndio haina Urai pacha.Kenya,Uganda,Rwanda Burundi wote wana Urai Pacha.
LIST OF AFRICAN COUNTRIES WITH DUAL CITIZENSHIP;
A. The current list of countries in Africa that have some form of Dual Citizenship:
1.Angola
2.Benin
3.Burundi
4.Cote d'Ivoire (restrictions on holding office as president & vice-president of the republic; president and vice-president of parliament - speaker and deputy speaker of parliament).
5.Djibouti
6.Egypt (with permission)
7.Eritrea (with permission , has created an intermediary status)
8.Gabon
9.Gambia
10.Ghana (Dual Citizens may not hold a set of listed senior positions, includes dual citizenship for the involuntary African diaspora . )
11.Kenya
12.Lesotho
13.Morocco
14.Mozambique
15.Namibia
16.Nigeria
17.Rwanda
18.Sao tome & Principie
19.Sierra Leone
20.South Africa (with permission/application at Dept. of Home Affairs)
21.Togo
22.Tunisia
23.Uganda
On the other hand, Tanzania Citizenship Act, 1995 on section 14 on Deprivation of citizenship of persons who exercise certain rights in other countries-stipulates- that The Minister may by order deprive any person, other than a person who is a citizen by birth, of his citizenship of the United Republic if the Minister is satisfied that person has at any time while a citizen of the United Republic and of full age and capacity voluntarily claimed and exercised, in a foreign country, any right available to him under the law of that country, being a right accorded exclusively to its own citizens, and that it is not conducive to the public good that he should continue to be a citizen of the United Republic.
http://www.refworld.org/docid/3ae6b5734.html
Post a Comment