ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, February 22, 2014

Misa ya Kiswahili - Kusherekea na Kuwaombea Wapendanao (Valentine

 Mapadri kutoka kushoto Fr. Shao, Fr. Leandrah Kimario na Fr. Jean Tambwe wakiongoza misa takatifu ya kiswahili iliyofanyika Baltimore, Maryland ya kuadhimisha miaka 3 ya misa ya Kiswahili DMV  hivi karibuni.

Wapendwa Wote

Mnakaribishwa sana kwenye ibada ya misa takatifu ya lugha ya kiswahili, kusheerekea na kuwaombea wapendanao (Valentine).
Ibada itafanyika katika kanisa takatifu katoliki la Mtakatifu Edward 


(St Edward Parish 901 Poplar Grove St Baltimore, MD 21216. Phone: (410) 362-2000 ).


Tarehe 23 Februari 2014, saa nane kamili mchana (2:00 PM).
Baada ya ibada tutakutana kwa mlo na viburudisho. 


Karibuni sana na unaombwa uwataarifu na kuwakaribisha ndugu na jamaa zako.
Asante sana kwa niaba ya Baba Evod Shao

No comments: