Na Rashid Nchimbi wa Jeshi la Polisi Arusha
Wananchi
Mkoani hapa wameonekana kuwa na muamko zaidi wa Ulinzi Shirikishi baada
ya kutoa taarifa mbili zilizofanikisha kukamata misokoto 1,038 ya
madawa ya kulevya aina ya bangi pamoja na mirungi kilogramu 75.
Akizungumza
na Waandishi wa habari ofisi kwake, Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa
Arusha Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP) Gilles Muroto alisema kwamba
katika matukio mawili yaliyofanikisha ukamataji wa madawa hayo taarifa
zake zilitolewa na raia wema.
Kaimu
Kamanda Muroto alisema kwamba, tukio la kwanza lilitokea tarehe
18.02.2014 muda wa saa 1:30 asubuhi maeneo ya Kituo Kikuu cha mabasi
jijini hapa ambapo mtu mmoja aitwaye Charles Ogaga Ayunga (38) raia wa
Kenya na ni mkazi wa Taveta nchini humo, alikamatwa na misokoto 1,038 ya
Madawa ya kulevya aina ya bangi iliyokuwa ndani ya boksi.
Akifafanua
taarifa hiyo Kaimu Kamanda huyo alisema kwamba, siku ya tukio mtuhumiwa
alikuwa anatokea maeneo ya Ngaramtoni akiwa kwenye Hiace na alipofika
maeneo ya Kituo Kikuu cha Mabasi alishuka akiwa na boksi na kutaka
kupanda basi linaloelekea Horiri wilayani Rombo lakini kabla
hajapandisha boksi hilo kwenye basi hilo watu walimshuku na kutoa
taarifa katika kituo kikuu cha Polisi, ambapo askari waliokuwa doria
maeneo ya karibu walikwenda katika maeneo hayo na kufanikiwa kumkamata
mtuhumiwa huyo akiwa misokoto hiyo.
Mara
baada ya mahojiano mtuhumiwa alikiri kuumiliki madawa hayo ya kulevya
aina ya bangi na kueleza kwamba alikuwa anasafirisha kupeleka nchini
Kenya.
Wakati huo huo mtu
mmoja aitwaye Philipo Santolin (25) Mkazi wa Horiri wilayani Rombo
alikamatwa na madawa ya kulevya aina ya mirungi yenye uzito wa kilogramu
75 ambayo ilikuwa imehifadhiwa kwenye vifurushi tofauti tofauti7.
Akifafanua
tukio hilo Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Mrakibu Mwandamizi wa
Polisi (SSP) Gilles Muroto alisema tukio hilo la ukamataji lilitokea
tarehe 19/02/2014 muda wa saa 2:00 usiku maeneo ya Kaloleni jijini hapa.
Alisema
siku ya tukio wananchi walitoa taarifa katika kituo kikuu cha Polisi
kwamba, kuna mtu alikuwa anasafirisha madawa hayo katika gari aina ya
Corolla lenye namba za usajili T 162 AYW toka mkoani Kilimanjaro kuja
Arusha, ndipo askari walipoweka mtego maeneo ya Kwa Mrefu na mara baada
ya gari hilo kusimamishwa halikusimama ndipo askari wakaamua
kulifuatilia ambapo walifanikiwa kulikamata maeneo ya Kaloleni mara
baada ya gari hilo la mtuhumiwa kupasuka tairi la mbele.
Kaimu
Kamanda Muroto alisema mpaka hivi sasa watuhumiwa wote wawili
wanahojiwa na watafikishwa makamani mara baada ya upelelezi kukamilika.

No comments:
Post a Comment