Na Veronica Kazimoto – MAELEZO
Ofisi
ya Taifa ya Takwimu imetoa wito kwa viongozi mbalimbali wakiwemo
wanasiasa wote nchini kutumia taakwimu sahihi zinazotolewa na Ofisi
hiyo ili ziweze kutumika katika kupanga mipango mbalimbali ya maendeleo.
Akizungumza na mwandishi wa habari
hii jijini Dar es Salaam, Meneja wa Teknolojia ya habari na Masoko
Bi.Mwanaidi Mahiza amesema Ofisi ya Takwimu imerahisisha upatikanaji wa
takwimu hizo kupitia Kanzidata inayoonesha viashiria vya kiuchumi na
kijamii (Tanzania Social Economic Database -TSED).
“Lengo
la kanzidata hii sio kuzibana Wizara wala kuwashurutisha wanasiasa
kutumia takwimu bali ni kuwarahisishia watumiaji wote wa takwimu kupata
taarifa kwa wakati pindi wanapokuwa katika kazi zao za kila siku,”
amesema Bi. Mahiza.
Meneja
huyo amefafanua kuwa TSED inasaidia kuondoa mlolongo wa upatikanaji wa
taarifa uliopo kwenye baadhi ya ofisi nyingi ambapo wakati mwingine
mteja huambiwa aaandike barua au arudi baada ya siku kadhaa.
Aidha,
amesisita kuwa ni muhimu kutumia Kanzidata hiyo kwa kuwa ndani yake
kuna takwimu rasmi ambazo zinatoka katika vyanzo sahihi vyenye mamlaka
ya kutoa takwimu hizo hapa nchini.
Bi.
Mwanaidi Mahiza ameyasema hayo wakati akikanusha habari iliyoandikwa na
moja ya gazeti la kila siku lililoripoti kuwa Ofisi ya Taifa ya Takwimu
kupitia marekebisho ya sheria ya takwimu ya mwaka 2002 ambayo yako
bungeni kutumika kuzibana wizara ili zitoe takwimu sahihi katika ripoti
zao kitu ambacho hakikuzungumzwa.
Hivi
karibuni baadhi ya wahariri na waandishi wa habari walipewa mafunzo na
Ofisi ya Taifa ya Takwimu juu ya Kanzidata inayoonesha viashiria vya
kiuchumi na kijamii (Tanzania Social Economic Database -TSED) ambapo
baadae moja ya gazeti la kila siku liliandika habari yenye kichwa cha
habari Ofisi ya Takwimu kuzibana wizara.
Kanzidata
inayoonesha viashiria vya kiuchumi na kijamii ilizinduliwa rasmi mwaka
2001 ikiwa na viashiria 75 ambapo hivi sasa ina viashiria 940 na
inapatikana katika mfumo wa DVD, CD ROMs na tovuti ya www.tsed.org.
No comments:
Post a Comment