Muwakilishi wa Kudumu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Tuvako Manongi akizungumza mwanzoni mwa Mkutano wa Mwezi mmoja wa Wajumbe wa Kamati Maalum ya Usimamizi wa Operesheni za Ulinzi wa Amani za Umoja wa Mataifa, (C-34). Katika baadhi ya mambo aliyosititiza ni pamoja na kuangaliwa upya kwa posho ya kila siku wanayolipwa walinzi wa amani ambayo ni dola 1.28, posho ambayo imedumu kwa miaka 20 bila ya kufanyiwa mabadiliko. Mkutano huo unafanyika hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa New York, Marekani. Aliyeketi nyuma kwa Balozi, ni Lt. Kanali Wilbert Ibuge Mwambata Jeshi katika Uwakilishi wa Kudumu.
Baadhi ya Waambata wa Kijeshi wanaoziwakilisha nchi zao Katika Umoja wa Mataifa, wakiwa katika picha ya pamoja muda mfupi kabla ya ufunguzi wa Mkutano wa Mwezi mmoja wa Kamati Maalum ya Usimamizi wa Operesheni za Kulinda Amani. Katika Mkutano huu wajumbe ambazo ni kutoka nchi ambazo zinachangia walinzi wa amani watajadili sera zote zinazohusu ulinzi wa amani chini ya Umoja wa Mataifa.
Na Mwandishi Maalum
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, imesema, posho ya dola 1.28 kwa siku wanayolipwa walinzi wa amani
wanaohudumu katika Misheni za kulinda amani za Umoja wa Mataifa, hailingani na
mazingira magumu na hatari ya
utekelezaji wa mamlaka wanayokabidhiwa na Umoja wa Mataifa.
Na kwa sababu hiyo ,na kwa zingatia hali halisi, Tanzania
imesisiza kwamba, wakati umefika
sasa wa kuangalia upya posho hiyo ambayo imedumu kwa zaidi ya miaka 20.
Balozi Tuvako Manongi, Muwakilishi wa Kudumu wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Umoja
wa mataifa, ametoa rai hiyo mwanzo mwa mkutano wa Kamati Maalum
ya Usimamizi wa Operesheni za
Ulinzi wa Amani maarufu kama C-34.
Kamati hii ambayo wajumbe wake ni kutoka nchi
zinazochangia walinzi wa Amani katika misheni mbalimbali za kulinda amani,
imeanza mkutano wake wa mwezi
mmoja hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa
ambapo wajumbe watajadili mambo yote yanayohusu sera za ulinzi wa
Amani chini ya Umoja wa Mataifa.
Balozi Manongi amewaeleza wajumbe wa mkutano huo kwamba
Kamati ilikuwa inaanza mkutano
wake, wakati ambapo , operesheni za ulinzi wa amani zinakabiliwa na changamoto mbalimbali zikiwamo za malipo duni.
“ Tunaposhindwa kukubaliana kujadili hoja ya kuongeza kiwango cha posho ya kila siku kwa
walinzi wa amani, posho ambayo
imebaki dola 1.28 kwa zaidi ya
miaka 20, siyo tu kwamba tumewaangusha walinzi wa amani, bali pia tunawavunja moyo na kuwakatisha
tamaa katika utekelezaji wa majukumu yao”. akasisitiza Balozi Manongi.
Akasema waeleza wajumbe licha
ya malipo duni na mazingira magumu,
walinzi hao wanajitolea uhai wao kwaajili
ya watu wengine na kwamba,kutokana umuhimu wao , Umoja wa Mataifa umejikuta
ukilazimika kuwapeleka katika Misheni ambazo ama hakuna amani ya kulinda
au mahali ambako kuna vikundi vingi vyenye silaha vinavyokinzana.
“Hii ndiyo hali halisi inayozikabili Misheni zetu
zote katika utekelezi wa mamlaka tunazokabidhiwa na Umoja wa Mataifa.
Inasikitisha na kukatisha tamaa pale
baadhi yetu tunaposisitiza kwamba Misheni mpya inayoundwa au kuongezewa mamlaka
itekeleze mamlaka hayo kwa kuzingatia rasilimali zilizopo, ili hali tunafahamu
wazi kwamba rasilimali zinazozungumzwa
ama hazipo au hazikidhi hali halisi ya
Misheni hizo”. Akabainisha Balozi Manongi
Na kuongeza.
“Ni vema tukaunganisha nguvu zetu kukabiliana na changamoto hizi na nyingine nyingi ili walinzi wa amani ambao wanategemewa sana waweze kusaidia katika ulinzi wa amani
kwa raia wasiokuwa na hatia, lakini pia
kujihakikishia usalama wao wenyewe.
Akaeleza kwamba
ni matumaini ya Tanzania kuwa hoja
ya kuongezwa kwa posho hiyo pamoja na nyongeza ya malipo ya vifaa itapewa umuhimu na kujadiliwa
ipasavyo katika mkutano ujao wa Kamati ya Tano ya Baraza Kuu la Umoja wa
Mataifa inayohusika na masuala ya
Utawala na Bajeti ya Umoja wa Mataifa.
Pamoja na
changamoto hizo, Muwakilishi huyo wa Tanzania, ameuhakikishia Umoja wa Mataifa kwamba, Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania itaendelea
kuwajibika kwa kushiriki katika operesheni za ulinzi wa Amani kwa
mujibu wa Mamlaka inayokabidhiwa na
Umoja wa Mataifa.
“ Tumedhamiria
na tunajivunia ushiriki wetu wa ulinzi wa Amani katika maeneo mbalimbali ikiwamo Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Kongo, ambako
tunashiriki kupitia Misheni ya
Kulinda Amani katika DRC ( MONUSCO). Misheni ambayo ndani yake kuna Force
Intervention Brigade ( FIB)”.
Vile vile akabainisha kwamba Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itaendelea kushiriki kikamilifu katika utekelezaji wa
Mpango Mpana wa Kisiasa wa Umoja
wa Mataifa, kuhusu Ulinzi, Usalama na Ushirikiano wa
Ki- maendeleo katika DRC na eneo
la Maziwa Makuu.
Akizungumzia
zaidi kuhusu Misheni ya MONUSCO
na mchango wake katika usimamizi wa amani katika DRC.
Balozi Tuvako Manongi amesema, Tanzania inaamini kwamba utendaji kazi wa Misheni hiyo unasimama katika misingi ya Misheni Moja,
Jeshi Moja, Nguvu Moja ya Mamlaka, kuwa ndiyo
mweleko sahihi na wenye tija katika ngazi zote kiutendaji.
Misheni ya MONUSCO
inaundwa na walinzi wa Amani kwa
upande mmoja kutoka Pakistani, India na
Bangladeshi pamoja na Tanzania,
Afrika ya Kusini na Malawi kupitia FIB.
Aidha,
Muwakilishi wa Tanzania katika
Umoja wa Mataifa, amezitaka Mamlaka za
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, kutumia
mafanikio yaliyopatikana hivi karibuni, kuimarisha taasisi zake za kisiasa, kiulinzi , kiuchumi pamoja
na kuongeza kasi ya majadiliano na maridhiano.
No comments:
Post a Comment