Watoto kwenye kampeni dhidi ya ukeketaji watoto wa kike na wanawake
Tarehe Sita Februari kila mwaka ni siku ya kimataifa ya kutokomeza ukeketeji wa watoto wa kike na wanawake. Takwimu zaonyesha kuwa kila mwaka watoto Milioni Tatu wako hatarini kukumbwa na mila hiyo potofu barani Afrika na huko Mashariki ya Kati inakotendwa. Shirika la idadi ya watu duniani, UNFPA linasema cha kutia shaka zaidi kitendo hicho sasa kinafanywa na baadhi ya wahudumu wa afya! Jambo hilo wanasema ni lazima ipigwe vita. Nchini Tanzania ukeketaji umeshika kasi zaidi huko Manyara, Dodoma, Arusha, Singida na Mara. Mwenzetu Noel Thompson wa Radio washirika Afya FM ya mjini Mwanza alipiga kambi huko Mara kujionea hali halisi.Ungana naye kwenye makala hii.
KUSIKILIZA BONYEZA HAPA
1 comment:
Aibu kwetu wauguzi huku tunajua madhara yake. Wamama wanachanika sana wakati wa kujifungua.
Post a Comment