Mahakama kuu Zanzibar leo imetoa dhamana kwa viongozi 10 wa jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kislamu --
Kwamba, dhamana hiyo imepatikana baada ya kupunguzwa masharti magumu ya kulipa fedha taslimu shilingi milioni 25 na badala yake, watuhumiwa watatkiwa kulipa kwa maandishi. Jaji wa Mahakama hiyo Fatma Hamid Mahmoud ametoa uamuzi huo na kusema kwa vile watuhumiwa wameshakaa ndani kwa muda mwingi mahakama imeona wana haki ya kupatiwa dhamna yenye masharti nafuu.
Jaji Fatma alikubali maombi yaliotolewa na mawakili wa watuhumiwa hao wakiongozwa na Salum Toufiq ya kila mshitakiwa kujidhamini mwenyewe kwa shilingi milioni 25 za maandishi, wadhamini wawili -- moja akiwa mfanyikazi wa serikali na kuwasilisha nyaraka za mali isiyohamishika.
Awali watuhumiwa hao walipewa masharti magumu ya kujidhamini ikiwemo kutoa fedha taslimu shilingi milioni 25, wadhamini watatu -- watumishi wa serikali, na mmoja wao awasilishe mali isiyohamishika -- masharti ambayo yaliwashinda na kulazimika kurudi tena ndani.
Watuhumiwa hao ni Faraidi Hadi Ahmed, Mselem Ali Mselem, Musa Juma Mussa, Azan Khalid Hamdan, Sleiman Juma Sleiman, Khamis Ali Sleiman, Hasan Bakari Sleiman, Gharibu Ahmada Juma, Abdalla Saidi na Majaliwa Fikirini Majaliwa.

Wote wanashtakiwa kwa makosa ya kuharibu mali, uchochezi, ushawishi na kuhamasisha fujo hapo mwezi Oktoba mwaka 2012.
Kesi hiyo imeahirishwa hadi Machi 27 mwaka huu kwa ajili ya kusikilizwa tena

inaripoti blogu ya Zanzibar Islamic News.
No comments:
Post a Comment