Na Masanja Mabula, PEMBA — JESHI la Polisi Mkoa wa Kaskazini Pemba,
linamshikilia mwanamke mmoja anayefahamika kwa jina la Mwanaisha Kiyaka
Ayoub (30) mkaazi wa Pande Tanga na Chake Chake kwa tuhuma za
kupatikana na mafurushi ya bangi.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi kwa niaba ya kamanda wa Polisi Mkoa huo, Mrakibu Mwandamizi wa Polisi, Mlenge Mohammed Mlenge, alisema mtuhumiwa alikamatwa jana majira ya saa 11:50 alfajiri baada ya kushuka kwenye mashua katika bandari ya Wete akitokea Tanga.
Alisema kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo kumetokana na ushirikiano uliopo kati ya wananchi na jeshi la polisi.

Taarifa za kwamba kuna mtu anakuja na bangi tulizipokea mapema na kuweka mtego hapa bandarini Wete, kwa kweli haikuwa shida kumkata
alisema.
Aidha alisema baada ya kufanya upekuzi kwenye begi lake walimkutana mafurushi 22 ya bangi.
Aidha alisema baada ya kufanya upekuzi kwenye begi lake walimkutana mafurushi 22 ya bangi.
Aliwataka wananchi kuendelea kuunga mkono falsafa ya polisi jamii ambayo
imekuwa msaada mkubwa katika kukabiliana na matendo ya uhalifu.
Alisema polisi wanaendelea kukamilisha uchunguzi kabla ya kumfikisha mahakamani. --- via ZanziNews
No comments:
Post a Comment