Katibu
Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue(Watatu kushoto) akiwa pamoja na
Viongozi wa Ikulu SACCOS wakati walipokwenda kujitambulisha na kukabidhi
ripoti ya utendaji ofisini kwake ikulu jijini Dar es Salaam leo.Wa
kwanza kushoto ni Mwenyekiti wa SACCOS hiyo Bwana Theofrid Kikombele,
Wapili kushoto ni Katibu wa SACCOS hiyo Bwana David Kivembele na kulia
ni mshauri mkuu wa SACCOS hiyo Bwana Joseph Sanga.
Viongozi
wa Ikulu Saccos wakiwa kwenye mkutano na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi
Ombeni Sefue ofisini kwake ikulu jijini Dar es Salaam leo.
(Picha na Freddy Maro.)
…………………………………………………………………………………………..
Na Freddy Maro. Ikulu.
Uongozi Mpya
wa ikulu SACCOS leo umejitambulisha rasmi kwa Katibu Mkuu Kiongozi
Balozi Ombeni Sefue, ikulu jijini Dar es Salaam na kukabidhi ripoti ya
utendaji ya SACCOS hiyo.
Waliojitambulkisha
kwa Katibu Mkuu Kiongozi ni pamoja na Mwenyekiti wa Ikulu SACCOS Bwana
Theofrid Kikombele,Makamu Mwenyekiti Bwana David Kivembele na Mshauri
Mkuu Bwana Joseph Sanga.
Akizungumza
mara baada ya kujitambulkisha, Mwenyekiti wa SACCOS hiyo Bwana Theofrid
Kikombele alisema uongozi huo umepanga mikakati madhubuti ya kuiendesha
SACCOS hiyo kwa uwazi na ufanisi zaidi ikizingatia kutenda kazi kwa
weledi na kuwahamasisha wafanayakazi wengi zaidi kujiunga.
Mkakati
mwingine, alisema Bwana Kikombele ni kwa SACCOS hiyo kuanzisha vitega
uchumi mbalimbali kwa lengo la kupanua mtaji ili kuweza kuwahudumia
vyema wanachama wa SACCOS hiyo kwa kuwawezesha kukopa zaidi kwaajili ya
shughuli zao mbalimbali za kujiletea maendeleo.
Wakati wa mkutano huo kati ya
Katibu Mkuu na Uongozi wa Saccos hiyo Viongozi hao walikabidhi ripoti ya
utendaji wa SACCOS hiyo na walimuomba Katibu Mkuu Kiongozi kujiunga na
SACCOS hiyo, ombi ambalo aliliafiki na kuahidi kutoa ushirikiano
kuboresha SACOSS hiyo.
No comments:
Post a Comment