ANGALIA LIVE NEWS

Friday, March 14, 2014

GARI LA WIZARA ZANZIBAR LAPINDULIWA KWA MAWE!-GPL

Habari zilizopatikana mchana huu kutoka visiwani Zanzibar zinasema kuwa vijana wenye mikokoteni inayovutwa na Ng'ombe wamefanya vurugu na kuanza kupiga mawe magari ya serikali huku wakijerui wafanyakazi wa serikali kadhaa. Katika kadhia hiyo, walisababisha gari la Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Uchumi, Mhe. Khamis Musa kupinduka kama linavyoonekana pichani. Inaelezwa kuwa chanzo cha vurugu hizo ni kupigwa marufuku kwa mikokoteni hiyo kuingia mjini, kitendo ambacho kinapingwa na wamiliki.

PICHA: Mdau, zanzibar

No comments: