
CHAMA CHA MAPINDUZI TAWI LA NEW- ZELAND
83 Grafton Road, Auckland, New -Zeland
March 30, 2014
YAH: TAMKO
KUHUSU HAKI ZA KUZALIWA ZA WATANZANIA ZETU ZA KUZALIWA KAMA WATANZANIAKATIKA
KATIBA YA MUUNGANO WA JAMHURI YA TANZANIA
Tawi la CCM New-Zealand, tunapenda
kutoa shukrani za kipee kwa Mwenyekiti wa CCM taifa, Mheshimiwa Rais Wa Jamhuri
wa Muungano wa Tanzania Mh. Dr. Jakaya Mrisho Kikwete kwa kuonyesha uongozi
uliotukuka wa kuitakia Tanzania katiba mpya ambayo itasaidia vizazi vya leo na
hata vya kesho. Kadhalika tunatoa shukrani za kipekee kwa Katibu Mkuu Ndg.
Ablrahaman Kinana, Katibu wa Uenezi na Itikadi Ndg. Nape Nauye kwa kuwa mstari
wa mbele kwa kuliendeleza chama
Uongozi wa wanachama wa Chama Cha
Mapinduzi tawi la New-Zeland, kadhalika tunapenda kuungana na watanzania
wenzetu wapenda maendeleo kote duniani kuwapongeza na kuungana na Ndg. John
Mashaka pamoja na Ndg. Kadari Singo mwakilishi wa wana Diaspora Katika Bunge La
katiba kudai haki zetu za kuzaliwa katika ardhi ya Tanzania. Tawi la CCM
New-Zealand Inawapongeza kwa Juhudi zenu za kuipigania Tanzania. Mmeonyesha ukomavu
na uongozi wa kweli
Uongozi wa CCM tawi la New-Zealand,
tunapenda kuwasilisha maombi ya wana CCM New-zeland kwa bunge maalum la Katiba.
Wana CCM New-Zealand wanaomba
watambulike na kupewa haki zao zote kama wazawa wa Tanzania. Tuna imani Chama
chetu sikivu, Chama chetu Makini cha CCM kitasimamia mchakato wa kutupa wana
New-Zeland na watanzania wengine duniani hii haki ya msingi, ya uraia.
CCM tawi la New-Zealand, tunapenda kuwahimiza
watanzania popote pale walipo duniani kushirikiana nasi katika mapambano ya
kudai hii haki ya kuzaliwa ya watanzania. Tuna imani Chama Makini Cha CCM
kitaongoza Mchakato wa kuwatambua Watanzania wote duniani
Ahsanteni,
Rajab M. Mrisho Tel: +64 9 356 2160
Mwenyekiti CCM, New-Zealand
No comments:
Post a Comment