Super woman katika Afro-Pop, Judith Wambura a.k.a Lady Jaydeee au Jide katika pozi na mume wake Gardner Habash ‘Kapteini’ .
Kumbe! Super woman katika Afro-Pop, Judith Wambura a.k.a Lady Jaydeee au Jide amefunguka kuwa yeye na mumewe, Gardner Habash ‘Kapteini’ kwa sasa wanaishi kama kaka na dada hivyo kuibua swali kivipi?
Akizungumza na Ijumaa Wikienda katika mahojiano maalum yaliyofanyika kwenye mgahawa wa staa huyo wa Nyumbani Lounge uliopo Ada Estate, Kinondoni jijini Dar mwishoni mwa wiki iliyopita, Jide alisema kuwa yeye na Gardner wamefikia hatua ya kuishi katika staili hiyo kutokana na mapenzi yao yaliyopitiliza.
“Gardner ananipenda sana na mimi pia vilevile nampenda sana mume wangu. Mapenzi yetu yamepitiliza hadi tunajiona kama vile tumezaliwa tumbo moja na ndiyo maana nawaambia kuwa mimi na yeye tunaishi kama kaka na dada,” alifunguka Jide.
Akiendelea kuzungumza kwa kujiamini, Jide alisema kuwa hadi simu ya mkononi wanatumia moja kwa ajili ya mawasiliano.
“Mimi hapa sina simu, anayo mume wangu lakini wakati mwingine nakuwa nayo mimi ila muda mwingi anakuwa nayo Gardner,” alimalizia Jide.
Kwa makala zaidi kuhusu usichokijua juu ya maisha ya Jide, nenda kurasa za nane na tisa za gazeti hili. GPL
4 comments:
Who cares?
we care kwa sababu haya ndo yanaitwa mapenzi ya dhati si mapenzi longa longa baba ndani ya nyumba anakuwa kama simba mama anakuwa kama panya hata kugusa simu yake unaogopa wangapi wanateseka majumbani katika ndoa zao na sometimes kidume kizima anachukua amri kutoka kwa mke wake na hana sauti kisa mkee analipa bili ndani ya nyumba yeye kavaa suruali kidume ameva suruli lakin anaushanga makalioni watu wawauoni ha ha ha what a joke
mapenzi kama haya ya jade na mumewe na adimu sama so mungu awabariki sana amen
nilivyosoma kichwa cha habari hii nikadhani duuu ebwana eeh mama sasa anakoromea jamaa kajajua mapenzi hampi na anasauti ya radi mbele ya mumewe nikawa na shauku sana ya kusoma ndo nilivyotafsiri akilini mwangu kwa nini asema yeye na mumewe ni kama dada na kaka lazima njemba amebanwa na furukuti na no game of love kumbe uandishi sometimes unazingua big up jade and gardien
usichukiye wala kupanda jazba mungu atakujalia na wewe kupata penzi la kweli na usiwe na wivu wa kusema who cares because mapenzi kama haya watu wanayalilia kila kona ya dunia na ni wachache sana huwa wanabarikiwa kuyapata katika dunia hii ya leo ya utapeli wa mapenzi kwa jinsi zote wanawake na wanaumme.
nakuombea mungu na najiombea mungu mimi mwenyewe pia tupate wapenzi wa kweli wa kufa na kuzikana itikiya basi amen
Post a Comment